Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TAIFA STARS

Tanzania yavunja mkataba na kocha Emmanuel Amunike

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jumatatu Julai 8 limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike. Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo. Shirikisho hilo pia limesema pia litatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN. "Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019," inasema taarifa ya TFF. Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja. Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39. Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria. Kocha hu...

AFCON: CAF YA TANGAZA BEI ZA KUONA MCHEZO HUKO MISRI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali za Africa (AFCON) zinazotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri. Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliyebebwa na wachezaji. Shrikisho la soka nchini TFF limethibitisha taarifa hiyo, ikisema kuwa CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali. Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la kwanza ni USD 29 ambayo ni sawa na takribani sh 66,700 za Kitanzania, tiketi za daraja la pili ni USD 18 ambazo ni sawa na sh 41,403 tiketi za daraja la tatu ni USD 6. Katika hatua ya makundi, Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja la kwanza ni  USD 35 ambayo ni takribani sh 80,521 kwa daraja la pili ni USD 24 na daraja la tatu ni ...