Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Osama vs marekani

Hamza Bin Laden: Mwana wa kiume wa Osama 'amefariki', yasema Marekani

Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo Mwana wa kiume wa muasisi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, Hamza,amefariki , kwa mujibu wa maafisa wa ujasusi wa Marekani. Taarifa kuhusu mahala au tarehe ya kifo cha Hamza Bin Laden bado haijawa wazi katika ripoti ya chanzo hicho cha habari. Mwezi Februari, Serikali ya Marekani iliahidi kutoa dola milioni 1 kwa ajili ya yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua ni wapi alipo. Hamza Bin Laden, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa ujumbe mbalimbali wa sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingine. Ripoti zilitolewa kwanza na mashirika ya habari ya NBC na New York Times. Hamza Bin Laden aliwatolea wito wapiganaji wa jihadi kulipiza kisasi mauaji ya baba yake aliyeuliwa na kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan mnamo mwezi Mei 2011. Kadhalika alikuwa amewatolea wito watu wa rasi ya A...

CIA yatoa faili 470,000 za Osama Bin Laden

Shirika la ujasusi la Marekani CIA limetoa karibu faili 470,000 zilizopatikana wakati wa kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden mwaka 2011. Faili hizo mpya ni pamoja na stakabadhi kuhusu mipango yake binafsi na video ya mtoto wake wa kiume Hamza wakati wa hasuri yake. Marekani kumsaka mtoto wa Osama Makamando wa Marekani wavamia al-Qaeda Yemen Hii ndiyo mara ya nne CIA inatoa faili za Osama zilizopatikana wakati wa uvamizi kwenye maficho yake huko Abbottabad nchini Pakistan. Hata hivyo faili zingine haziwezi kutolewa kwa sababu zinaweza kuathiri usalama wa tiafa. Kulingana na CIA faili hizo zinafichua uhusiano uliopo sasa kati ya al-Qaeda na ISIS na migawanyiko kati ya al-Qaeda na washirika wake. Kampiuta iliyopataiaka wakati wa uvamizi huo ilikuwa na filamu za Hollywood, vipindi vya watoto na makala tatu kumhusu Osama Bin Laden. Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani Video nyingine ni ya harusi na mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden akiwa mdogo. Hamza Bin...