Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Paul Kagame

Victiore Ingabire na Kizito Mihigo waachiliwa huru na rais Paul Kagame Rwanda

Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu. Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010. Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa. Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri. Taarifa ilisema kuwa bwana Kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama rais. Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10...

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakutana Mauritania

Viongozi wa  Afrika wanakutana Mauritania Jumapili(01.07.2018)katika mkutano wa siku mbili utakaolenga biashara huria, upatikanaji wa fedha, mapambano dhidi ya rushwa pamoja na mizozo mingi  ya kiusalama barani humo. Zaidi  ya  viongozi  wa  serikali  na  taifa  40 wanatarajiwa  kuwasili  katika  mji  mkuu  wa Mauritania  , Nouakchott, wakiungana  siku  ya  Jumatatu na  rais  wa  Ufaransa  Emmanuel Macron , ambaye  anatarajiwa  kusukuma juhudi  za  kiusalama  katika  eneo  la  Afrika kaskazini. Kiongozi  wa  Rwanda  Paul Kagame, ambaye anashikilia  urais wa  kupokezana  wa  Umoja wa  Afrika  ( AU )wenye  wanachama  55, atatoa  rai  kuhimiza  biashara  huru. Paul Kagame (kulia) akisalimiana na ...