Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TP MAZEMBE

Mo Dewji atuma salaam Al Ahly, Esperance na Mamelodi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa klabu hiyo itashindana na timu kubwa barani Afrika msimu ujao katika dirisha la usajili. Mohamed Dewji Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Jumamosi hii, Mo Dewji amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku huku kutokana na kukamilika kwa mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji na kupanuka kwa vyanzo vya mapato ya klabu. " Mwaka juzi ukilinganisha na mwaka jana, bajeti yetu imekuwa ikizidi kwa asilimia 60 hadi 70 na mwaka huu bajeti unazidi. Kwakuwa mabadiliko yamefanyika vizuri, tumeanza kupata vyanzo vingi vya mapato ", amesema Mo. " Kiujumla tumejitayarisha kushindana na hizi klabu kubwa na kusajili wachezaji wazuri. Tayari kuna kamati maalum ambayo inalifanyia kazi suala la usajili, kuna wachezaji wengi mikataba yao inaisha. Wengi tutaendelea nao na wengine tutawaacha. Kwahiyo tutakuwepo kwenye ...