Viongozi wa Afrika wanakutana Mauritania Jumapili(01.07.2018)katika mkutano wa siku mbili utakaolenga biashara huria, upatikanaji wa fedha, mapambano dhidi ya rushwa pamoja na mizozo mingi ya kiusalama barani humo. Zaidi ya viongozi wa serikali na taifa 40 wanatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Mauritania , Nouakchott, wakiungana siku ya Jumatatu na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron , ambaye anatarajiwa kusukuma juhudi za kiusalama katika eneo la Afrika kaskazini. Kiongozi wa Rwanda Paul Kagame, ambaye anashikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Afrika ( AU )wenye wanachama 55, atatoa rai kuhimiza biashara huru. Paul Kagame (kulia) akisalimiana na ...