Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WORLD BANK

Watanzania washauriwa kukopa

Dkt. Mwakyembe : Woga wa kukopa ni tatizo kubwa kwa Watanzania Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema Watanzania waache kuogopa kukopa lakini benki nazo zibadilike.  Dkt. Mwakyembe amesema, woga wa kukopa ni tatizo kubwa kwa Watanzania na ni la kihistoria kwa kuwa zamani kuliko na sheria iliyowazuia wazawa wasikope kwa sababu iliwatambua kuwa ni watoto.  Waziri Mwakyembe amewaeleza wajumbe wa Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoa wa Tabora hali sasa imebadilika hivyo wananchi wakope wawekeze.  Tabora inabidi ibadilike hasa, isiwe Tabora ile ya maembe tunagawana na wadudu” amesema na pia amewaeleza viongozi kuwa uongozi si umasikini.  Dkt. Mwakyembe amesema, viongozi hawazuiwi kuwa matajiri ila watapaswa kueleza wameupata vipi utajiri huo na ndiyo maana kuna suala la maadili kwa viongozi wa umma.  Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora lililofanyika kwa siku tatu mjini Tabora. Waz...

Benki ya Dunia yamwaga Tanzania shilingi Bilioni 680.5 za utekelezaji miradi ya maendeleo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi Bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, nyumba za watumishi na kununua vifaa vya kufundishia.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es SalaamMakamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem aliyekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 16 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na kuridhia kutoa fedha za mradi huo, Benki hiyo inaendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nch...