Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Al Hilal

Patrick Aussems akabidhiwa jina la mshambuliaji wa Al Hilal

Kocha wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ameweka wazi kuwa amekabidhiwa jina la mshambuliaji Thomas Ulimwengu.  Ulimwengu ambaye amevunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan anatajwa kutakiwa na Simba kwa ajili ya kumtumia kwenye michuano ya kimataifa.  Mshambuliaji huyo alikuwa na Taifa Stars nchini Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika lakini hakuweza kucheza kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike kumuweka benchi.  Ulimwengu amecheza mechi mbili tu chini ya Amunike ambazo zilikuwa ni dhidi ya Uganda na ile mechi ya kwanza ya Cape Verde, hivyo Mbelgiji alitegemea amuone akicheza na Lesotho lakini haikuwa hivyo.  Awali chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kililiambia Championi Jumamosi kuwa, klabu hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kutaka kumsaini lakini kwa sasa inaonekana kama unaelekea kukwama kutokana na kocha kutomuona Ulimwengu akicheza licha ya kuambiwa ni mchezaji mzuri.  “Usajili wa Ulimwengu ba...