Neymar ameifungia PSG mabao 23 katika mechi 28 msimu huu Real Madrid imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27. (Sky Sports) Azma ya Barcelona kumsajili tena Neymar, 27, inategemea ikiwa klabu hiyo itamuuza Philippe Coutinho ambaye pia ni mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Brazil. (Goal) Manchester United wako tayari kulipa £81m ambayo itawawezesha kumnyakua mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Bilbao Inaki Williams, 25. (El Chiringuito TV - via Mail) Pendekezo la Leroy Sane kuhamia Bayern Munich kutoka Manchester City limeathiriwa na jeraha la goti linalomkabili nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Mail) Leroy Sane (Kulia) Beki wa Chelsea Mbrazil David Luiz, 32, ataruhusiwa kujiunga na Arsenal kwa £8m tu. (Mirror) Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,26, amewasilisha ombi la kutaka uhamisho huku kukiwa na tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast akipingiwa upatu kuhamia...