Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Chimbuko la mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylian Mbappe


Lionel Messi na Kylian Mbappe walipokumbatiana kipenga cha mwisho baada ya mechi yao, ilitoa taswira ya kupokezana kwa kijiti cha ubora kutoka nyota hadi mwingine.


Kila mmoja aliyehudhuria mchuano huo wa kukata na shoka, aliaga uga wa Kazan Jumamosi akihisi kushuhudia mechi spesheli itakayosalia akilini kwa miaka.

Kwa kifupi, ni mchezaji mmoja alichukua sifa zote siku hiyo

Mbappe ana umri wa miaka 19 tu lakini amefunga mabao mawili muhimu na kuchomoka kwa kasi kutoka kitovu cha uwanja na kupelekea penalti iliyoipa Ufaransa bao la ufunguzi wakati ilipoichabanga Argentina 4-3.

Ushindi huo umewafikisha vijana wenye vipawa wa Didier Deschamp robo fainali.

Ni maonyesho yaliyofichua uwezo kamili wa Ufaransa kufika fainali Urusi 2018 na kuondoka na Kombe la Dunia kwa mara ya pili.

Mbappe - Mshambulizi mwenye ukwasi wa talanta

Mbappe hakuzaliwa Ufaransa ilipotwaa Kombe la Dunia ikiwa nyumbani 1998.

Cha kustajaabisha, Mbappe alifufua kumbukumbu za mchezo wa Michael Owen na usumbufu wa mfungaji huyo wa Uingereza dhidi ya mabeki wa Argentina 1998, yaani miaka 20 tangu Juni 30 1998.

Mbappe, aliyezaliwa Disemba 20 1998, anatarajiwa kujiunga na PSG licha ya kuwatumikia kwa mkopo kutoka Monaco.

Atajiunga na mabingwa hao wa Ufaransa kwa Euro Milioni 180m na kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kwa bei ya juu baada ya mwenzake wa kikosi cha PSG, Neymar kununuliwa kwa Euro milioni 200 mnamo 2017.

Mbappe amebarikiwa na kasi, ujasiri, kujiamini, uwezo wa kutumia miguu yote, utulivu, na uhodari mbele ya lango.

Mabao yake mawili dhidi ya Argentina yalidhihirisha haya.

"Ukiwa na miaka 19, kuonyesha tajriba na kuandaa maonyesho aina hiyo mbele ya mamilioni na Messi akiwemo, ni bidii na kongole." Alisema Alan Shearer.

Mbappe, kutoka mitaa ya Paris, aliitwa timu ya taifa mwaka uliopita pekee.

Ukuaji wake umekuwa ni wa kasi tangu alipojitokeza msimu wa 2016-17, alifunga magoli 26 mechi 44 na kuiwezesha Monaco kutua nusu-fainali za Champions League na kulitwaa taji la Ligue 1.

Mabao yake mawili yalizima taa za Argentina zilizoanza kuwaka Urusi na kujitambulisha kwenye ulingo wa soka duniani.


Ni 1958 tu wakati mchezaji mkongwe wa Brazil Pele, akiwa na miaka 17, alipoifunga Sweden magoli mawili mechi ya fainali, ndio mchezaji chipukizi ametandika mabao mawili wavuni mechi moja Kombe la Dunia.

"Nimejawa na furaha, na ni uchochezi kumithilishwa na mchezaji wa kiwango cha Pele, yeye yuko katika kitengo tofauti," Mbappe alidai.

"Bado, ni jambo kubwa kuingia orodha ya wachezaji waliofanikiwa kiwango hicho." Alizidi.

Kylian Mbappe na Lionel Messi

Lionel Messi hajawahi kusajili bao hatua ya mchujo Kombe la Dunia.

Ngarambe dhidi ya Ufaransa ilitonesha na kukifungua kidonda cha zamani cha Messi, mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or anayeonekana kutapatapa kwenye jukwaa kubwa la soka.

Kipenga cha mwisho kilipolia ugani Kazan, Messi hakuangalia nyuma baada ya kukumbatiana na Mbappe.

Alichangia mabao mawili ya Argentina mechini, ikiwemo kumlisha Aguero, na kupiga shuti lililoelekezwa langoni na Gabriel Mercado wakati walichukua uongozi mechini.

Haki miliki ya pichaMBAPPEImage captionMbappe alikuwa akiewka picha za Ronaldo katika chumba chake

Alifunga bao la ajabu dhidi ya Nigeria walipokuwa kifua mbele dhidi ya Nigeria.

Messi amesema Urusi imemwacha na uchungu Zaidi ya yote hata baada ya Ujerumani kuwapiku kwa Kombe la Dunia 2014, na kupoteza dhidi ya Chile fainali za Copa America mnamo 2015 na 2016.

Messi aliwahi kutangaza kustaafu mwaka wa 2016 baada ya kufungwa lakini alibadili mawazo na kuwapiga jeki wenzake kufuzu kushiriki Urusi alipofunga mabao matatu dhidi muhimu dhidi ya Ecuador.

Kombe la Dunia sasa ndilo pengo lililosalia moyoni Messi tofauti na Maradona aliyebeba mwaka wa 1986.


Mwisho wa zamu ya Argentina?

Haki miliki ya pichaJOHN BENNETT

Kizazi cha sasa cha Argentina kilibeba kombe la dunia kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 1995, 1997, 2001, 2005 na 2007, lakini sasa wankabiliwa na uhaba wa mastaa wa vizazi vijavyo.

Pigo dhidi ya Ufaransa huenda ikamua hatma ya kocha Argentina Jorge Sampaoli. Baada ya kutotimiza matarajio, wengi wanahisi awamu yake imekatika!

Tayari nahodha Javier Mascherano ametangaza kustaafu kwake.

AKiwa na miaka 34, Mascherano ndiye mwenye umri wa juu Zaidi kizazi hiki Argetina.

Ifikapo Kombe la Dunia 2022, Sergio Aguero, Gonzalo Higuain na Angel di Maria watageuka 34.

Ufaransa haikabiliwi na shida hiyo.

Mshambulizi wa Barcelona mwenye umri wa miaka 21 Ousmane Dembele alikuwa kwenye benchi, Antoine Griezmann ana miaka 27 na kuna matumaini kwa Paul Pogba aliye na miaka 25.

Alexandre Lacazette, Kingsley Coman, Adrien Rabiot na Anthony Martial wamechwa nje ya kikosi cha sasa.

Mbappe akiendelea kuonyesha matokeo namna laivyofanya Jumamosi, Dimba hili liageuka kuwa spesheli kwake na kwa Ufaransa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...