Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Watu 20 wafariki dunia katika ajali ya barabarani Mbeya, Tanzania

Takriban watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha zaidi ya magari matatu mkoani Mbeya, kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania.


Ajali hiyo ilitokea katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya.


Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40.



Mnamo 14 Juni, watu 13 wakiwemo vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya.


Aprili, watu wanane waliokuwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah walifariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi katika eneo la Igodima. Gari hilo lililokuwa likitokea Chunya kwenda Mbeya mjini, lilikuwa na abiria tisa waliokuwa wakienda katika msiba wa ndugu yao.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna msaidizi Musa Athumani Taib ameambia BBC kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo ya Jumapili.


Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lililokuwa limebeba kontena lenye shehena ya mzigo, lilikuwa linatokea Mbeya Mjini kwenda Tunduma kugongana na mabasi madogo ya abiria matatu, ambapo moja lililaliwa na lori hilo lenye kontena baada ya kugongwa na kutumbukia mtoni katika eneo la Iwambi, Mkoani Mbeya.


Mabasi hayo madogo ya kuwabeba abiria maarufu kama Daladala ambayo yalihusika kwenye ajali hiyo hufanya safari zake kati ya Mwanjelwa na Mbalizi.


Miongoni mwa waliofariki dunia ni wanaume 10 na wanawake 10 akiwemo mtoto mmoja.


Akitoa salamu za rambi rambi kufuatia ajali hiyo, Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya ajali hiyo.



Rais wa Tanzania John Magufuli

Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu, Rais Magufuli amewataka viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine zinazohusika katika udhibiti wa usalama wa barabarani kujitafakari na kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na ajali hizo.



''Inauma sana kuwapoteza idadi hii kubwa ya Watanzania wenzetu katika ajali za barabarani ambazo tunaweza kuziepuka. Nawapa pole familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo vya Watanzania wenzetu hawa, sote tuwaombee Marehemu wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi wapone haraka," amesema Rais Magufuli katika taarifa hiyo.


"Haikubaliki hata kidogo kuendelea kupoteza roho za watu katika ajali tunazoweza kuzizuia," ameeleza.


Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40.


Aprili mwaka huu, baada ya kutokea kwa ajali nyingine Taboras, Rais Magufuli alikuwa amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale.


Aidha, aliwataka kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.


Ajali mbaya zilizoikumba Tanzania 2018, Magufuli alisema nini?


Kumekuwa na msururu wa ajali mbaya za barabarani na za nyingine zilizohusisha treni ambazo zimewaua watu zaidi ya 10 kwa wakati mmoja nchini Tanzania, mbili za karibuni zikiwa hizo zilizowaua watu takriban 40 katika mkoa wa Mbeya.


14 Januari, 2018: Watu 11 wafariki Kagera


Watu 11 walipoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Nyangozi, Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.


Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 jioni baada ya basi dogo la abiria aina ya Nissan Caravan lililokuwa likitoka Kakonko Mkoani Kigoma kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga kuligonga ubavuni lori la mizigo kisha kugongana uso kwa uso na lori jingine na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 6 kujeruhiwa.


Rais Magufuli alisema: "Nimehuzunishwa na kusikitishwa sana na vifo hivi, nawapa pole wafiwa wote, ninawaombea marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku". Aliwakumbusha watumiaji wa barabara hasa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.


Aidha liviagiza vyombo vinavyohusika kuongeza jitihada za kukabiliana na ajali za barabarani ili kuokoa maisha ya watu na mali zinazopotea kutokana na ajali.


24 Machi, 2018: Watu 26 wafariki Mkuranga Mkoani Pwani


Watu 26 walipoteza maisha na tisa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga Mkoani Pwani saa 3 usiku, baada ya basi dogo (Hiace) lililokuwa limebeba abiria kugongana na lori lililokuwa limebeba chumvi katika kijiji cha Mparange.


Basi hilo lilikuwa linatoka Mkuranga kuelekea Kimanzichana wakati lori lilikuwa linatoka Lindi kuelekea Dar es Salaam.


Rais Magufuli Rais Magufulialivitaka vyombo vinavyoshughulikia usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili.


4 Aprili, 2018: Watu 12 wafariki Tabora


Watu 12 walipoteza maisha na 46 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.


Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.


Rais Magufuli aliwataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.


"Nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na Mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani," alisema.


6 Juni, 2018: Basi la abiria lagongana na treni Kigomana kuwaua watu 10


Watu 10 walifariki baada ya basi la abiria kugongana na treni ya mizigo Mjini Kigoma majira ya saa 12:15 asubuhi katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.


Ajali ilitokea wakati basi la abiria la kampuni ya Prince Hamida lililokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda Tabora lilipoigonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.



Magufuli alisema: "Kwa mara nyingine tumewapoteza Watanzania wenzetu 10 katika ajali, tumepoteza wapendwa wetu na tumepoteza nguvu kazi ya Taifa, nawakumbusha wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi, vyombo husika chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani."


14 Juni, 2018: Watu 13 wakiwemo vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wafariki dunia


Vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya.


Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la abiria la kampuni ya Igunga Trans walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kisha kupinduka katika eneo la Mwansekwa. Vijana hao wa JKT walikuwa safarini kutoka Tabora kwenda Kikosi cha JKT Itende Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo ya JKT.


Rais Magufuli alisema: "Nimeumizwa sana na vifo vya vijana hawa".


25 Juni, 2018: Watu 14 wafariki ajali ya basi na lori Mkuranga, Pwani


Watu 14 walipoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kubebea mchanga katika eneo la Dundani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.


Wanne walijeruhiwa.


Ajali hiyo ilitokea saa 10:40 Alfajiri wakati basi dogo lililowabeba wanafamilia, ndugu na jamaa waliokuwa wakielekea Msata kuhudhuria sherehe za kumaliza mafunzo ya kijeshi kwa mtoto wao, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Dundani kuchukua mchanga.


Rais Magufuli alituma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kusema "Naomba unifikishie pole nyingi kwa wanafamilia wote waliopatwa na msiba, waambie naungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya kuondokewa na wapendwa wao, na sote tuwaombee Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi".


1 Julai 2018: Watu 20 wafariki ajalini eneo la Iwambi, Mkoani Mbeya.


Watu 20 walifariki baada ya Lori (nusu-trela) kuyagonga mabasi madogo ya abiria 3 likiwemo 1 lililolaliwa na trela hilo lenye kontena baada ya kugongwa na kutumbukia mtoni katika eneo la Iwambi, Mkoani Mbeya.




Lori hilo lilikuwa linatokea Mbeya Mjini kwenda Tunduma (katika barabara ya Dar es Salaam - Tunduma - Zambia) na mabasi madogo ya abiria (Daladala) yalikuwa yanafanya safari zake kati Mwanjelwa na Mbalizi.


Magufuli alisema: "Haikubaliki hata kidogo kuendelea kupoteza roho za watu katika ajali tunazoweza kuzizuia."


Aliwataka viongozi wa Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine zinazohusika katika udhibiti wa usalama wa barabarani kujitafakari na kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na ajali hizo


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...