Mabadiliko baraza la mawaziri Tanzania: Magufuli amfuta kazi Mwigulu Nchemba, Zitto Kabwe na Pole Pole walumbana


Mwigulu Nchemba

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri chini ya kipindi cha mwaka mmoja


Aliyeathirika na mabadiliko ya Rais Magufuli siku ya Jumapili ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.


Mwigulu Nchemba alipata umaarufu kwa juhudi zake za kuzuia maandamano dhidi ya Rais Magufuli.


Alinukuliwa akitishia kuwalemaza waandamanaji na ''kuwakamata hata watakaoandamana wakiwa nyumbani".




Licha ya hapo awali kuhamishwa kutoka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, hadi wadhfa wake wa mwisho, Nchemba ameondolewa baada ya kuhudumu kwa miaka miwili katika baraza la Rais Magufuli.


Mbunge huyo wa Iramba aliyechukua nafasi ya aliyekuwa waziri Charles Kitwanga, sasa atampisha mbunge mwenzake kutoka Jimbo la Mwibara, Kangi Alphaxard Lugola kujaza pengo hilo.



Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe

Lugola amepandishwa wadhfa kutoka ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira ambapo alikuwa naibu waziri. Nafasi yake imechukuliwa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mussa Ramadhani Sima.


Katika mabadiliko mengine , Waziri Makame Mbarawa aliyesimamia wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amebadilishana wadhifa na mwenzake wa wizara ya maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe.



Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @hpolepole

Vilevile wizara ya kilimo imeongezewa naibu waziri moja zaidi.


Mbunge wa Morogoro kusini mashariki Omary Tebwete Mgumba ameteuliwa kushirikiana na Dkt. Mary Mwanjelwa aliyekuwa naibu pekee kwenye Wizara hiyo.


Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amehamia tume ya taifa ya uchaguzi NEC lakini amedumisha cheo chake kwani ameteuliwa kuwa mkurugenzi katika tume hiyo.




Athumani amepata mwanya baada ya aliyekuwa akishikilia wadhfa huo, Ramadhani Kailima kupandishwa ngazi hadi naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi.



Rais Mgufuli na Mwigulu Nchemba

Ingawa waziri wake ameng'olewa, Balozi Hassan Simba Yahya, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, amepata nafuu kwa kupewa ubalozi huku Ikulu ikiahidi kufafanua kituo chake cha kazi hapo baadaye.


Uteuzi mwingine ni wa viongozi mbalimbali wa taasisi za idara tofauti za serikali.


Maafisa hawa wataapishwa siku ya Jumatatu katika Ikulu ya rais.


Mabadiliko haya yanajiri baada ya Rais Magufuli kuzidisha idadi ya wizara kwenye serikali yake kutoka 19 hadi 21 alipotenganisha wizara ya Nishati na Madini na kilimo na ile ya mifugo na uvuvi


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU