Je ni kweli uhaba wa samaki katika Ziwa Tanganyika unatokana na kupuuza mila na desturi? Nchini Tanzania uvuvi hunufaisha zaidi ya watu milioni nne, huku wakaazi wa mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania wakiutegemea kama shughuli kuu inayoendesha Maisha yao kiuchumi. Hata hivyo shughuli hiyo katika eneo hilo kwa sasa inaenda kombo kutokana na uhaba wa samaki kwenye ziwa Tanganyika huku baadhi ya wavuvi wakiamini kuachwa kwa mila na desturi ni moja ya sababu inayochangia uhaba wa samaki. Jitihada ni kubwa, mavuno madogo, wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu. Miezi kadhaa iliyopita wavuvi walikuwa wakipata zaidi ya ndoo ishirini za samaki, lakini kwa sasa mambo ni tofauti. Wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu. Wavuvi wengine wameamua kuachana na kazi hii na kuingia kwenye kilimo huku baadhi yao wanaona kuzipa kisogo mila na desturi ndio huchangia uhaba wa samaki katika ...