Je ni kweli uhaba wa samaki katika Ziwa Tanganyika unatokana na kupuuza mila na desturi?
Nchini Tanzania uvuvi hunufaisha zaidi ya watu milioni nne, huku wakaazi wa mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania wakiutegemea kama shughuli kuu inayoendesha Maisha yao kiuchumi.
Hata hivyo shughuli hiyo katika eneo hilo kwa sasa inaenda kombo kutokana na uhaba wa samaki kwenye ziwa Tanganyika huku baadhi ya wavuvi wakiamini kuachwa kwa mila na desturi ni moja ya sababu inayochangia uhaba wa samaki.
Jitihada ni kubwa, mavuno madogo, wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu.
Miezi kadhaa iliyopita wavuvi walikuwa wakipata zaidi ya ndoo ishirini za samaki, lakini kwa sasa mambo ni tofauti.
Wanawake wamefika ufukweni asubuhi na mapema kuchuuza samaki lakini upatikanaji ni adimu.
Wavuvi wengine wameamua kuachana na kazi hii na kuingia kwenye kilimo huku baadhi yao wanaona kuzipa kisogo mila na desturi ndio huchangia uhaba wa samaki katika ziwa hili.
Dunia Rashid ni mvuvi katika eneo hili anasema: 'Tunaweza kuchukua mwaka mzima tunavuwa samaki kama dagaa na samaki wakubwa wakubwa.
'Basi wale waliokuwepo, wazee wametoweka wengine, wamebaki vijana wadogo, shughuli hawawezi kuzifanya.'
Wazee wa kimila wanasema asiyesikia la mkuu huvunjika mguu, wananyooshea vidole teknolojia kama chanzo cha vijana wengi kuachana na mila na desturi ambazo huamini ndio njia pekee ya mafanikio.
'Machifu walikuwa wanafanya matambiko, wanaomba dua kwa MwenyeziMngu kutumia mambo ya asili, na kweli MwenyeziMngu alikuwa anatoa jibu.
Moshi Haruna ambaye ni mvuvi, anawaelemisha wavuvi wenzake dhidi ya kuamini kuwa mila ndio husababisha uhaba wa samaki
Mboga zilikuwa zinavulika na kupatikana,' anasema mzee Muhsini Mmbanga.
Katika mkusanyiko ulio mfano wa kanisa ila sio kanisani, Moshi Haruna, mvuvi mwingine katika eneo hili anawaelemisha wavuvi wenzake dhidi ya kuamini kuwa mila ndio husababisha kushindwa kupata mavuno ya samaki.
'Wale wanaoendekeza mila, wanaamini kwamba bila ya mila hawawezi kupata. Ila sisi ambao hatuamini mila tunaamini, Mungu anatoa kulingana na vile anaona awalisheje binaadamu.
Kwa wa mila wanakula, na sisi ambao hatuamini mila tunakula na tunaishi' anaeleza Haruna.
Mamlaka za serikali zinazoshughulikia uvuvi katika ziwa hili, zinasema uhaba wa samaki kwa msimu huu sio jambo lakiimani.
Edimund kajuni-ni afisa wa uvuvi Kigoma: 'Kwa uhalisia ni kwamba katika ziwa Tanganyika tuna misimu mitatu ya uvuvi'.
'Kuna kipindi ambacho ni msimu mb'aya, ambao ndio msimu tuliopo hivi sasa unaoanza mwezi wa tano Mei hadi wa saba Julai' anaeleza Edimund, afisa uvuvi Kigoma.
Uvuvi katika Ziwa Tanganyika
Imani potofu, dhana duni za uvuvi ni moja ya sababu zinazotajwa kurudisha nyuma sekta ya uvuvi nchini Tanzania.
Baadhi wanaona jitihada zaidi zinahitajika kuifanya sekta hii iweze kuinufaisha jamii na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa
Maoni