WAZIRI MKUU AELEKEA BELARUS KWA ZIARA YA KIKAZI
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, leo Julai 20, 2025 ameondoka nchini kuelekea nchini Belarus kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu. Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kukuza fursa za kiuchumi kati ya Tanzania na Belarus. Katika ziara hiyo, Mhe. Majaliwa anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Belarus, Alexander Turchin ambapo watajadili masuala ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu,Kilimo na viwanda. Waziri Mkuu pia atapata fursa ya kutembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa nchini humo cha Republican Unitary Production Enterprise na kujionea mbinu za kisasa za uzalishaji wa bidhaa za afya. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia atatembelea kiwanda cha matrekta cha Minsk Tractor Works JSC pamoja na chuo kikuu cha Agrarian State University Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kufanya mikutano ya uwili itakayojumuisha viongozi wa kiserikali na Chama cha wafanyabiashara wa Belarus cha AFTRADE. Lengo la mikutano ...