Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatahadharisha Wabunge wake kwamba endapo wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge hilo huku akiwakumbusha wengine wanaweza wasirudi kwenye mjengo huo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiwakumbusha wabunge kazi waliyonayo leo itakapofika saa 11 jioni ambayo itakuwa kupiga kura ya kuipitisha bajeti. “Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, bunge hili Rais atalivunja haraka. Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako .” amesema Spika Ndugai. B Mbali na hayo Ndugai amewasisitiza wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11 na kuwakumbusha kuwa kura haipigwi kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti. Wabunge wanatarajia kupigia kura bajeti ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia TSh32...