mteulethebest Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi. -Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup. -Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45. -Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12. -Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabw...