Real Madrid wana imani watafanikiwa kumsajili kiugo wa kati Mfaransa Paul Pogba kutoka Manchester United msimu ujao. (ESPN) Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajiliwa wa winga wao wa miaka 23 Mjerumani Leroy Sane, amabaye thamani yake inakadiriwa kuwa £90m. (Mirror) Romelu Lukaku, 26, amesafiri nyumbani Ubelgiji siku ya Ijumaa kufanya mazungumzo na ajenti wake huku Inter Milan wakikaribia kufikia mkataba wa £70m kumnunua kuingo huyo wa safu ya ushambulizi kutoka Manchester United. (Daily Mail) Romelu Lukaku akiwa mazoezini na wachazaji wenzake Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amesema chamsingi ni maishani ni "pesa kwanza kisha klabu baadae" kwa maneja wake wa zamani Rafael Benitez, na kuongeza kuwa "ni vigumu" kuendelea kumng'ang'ania raia huyo wa Uhispania. (Mail) Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid. (Independent) Mshambuliaji ...