Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani


Ronaldo, atakuwa na miaka 33 mwaka huu, na alitawazwa mchezaji bora duniani miaka 4 kati ya tano iliyopita


Cristiano Ronaldo amefunga mabao 58 miaka miwili iliyopita na kuwasaidia Real Madrid kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili mtawalia na pia La Liga mara moja.


Miaka hiyo miwili iliyopita, ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani, tuzo ya Ballon D'Or, mtawalia.


Anafaa basi kuwa mchezaji bora zaidi duniani na thamani yake kuwa ya juu zaidi?


Ni kweli uchezaji wake hauna kifani. Lakini kwa thamani, la hasha.


Utafiti huo wa shirika la takwimu za michezo la CIES


Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la takwimu za michezo la CIES iliyotolewa Jumatano, mchezaji huyo ni wa 49 kwa thamani duniani.


Anayeongoza orodha hiyo ni mshambuliaji wa Paris St-Germain ya Ufaransa, Mbrazil Neymar, 25, ambaye ndiye mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na klabu yoyote duniani na mwenzake wa Barcelona Lionel Messi, 30, kutoka Argentina.


Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ameorodheshwa kuwa wa tatu.


Unaweza kushangaa ni kwa nini thamani ya Ronaldo imekadiriwa kuwa $96,6 milioni.


Utafiti wa mwaka jana wa CIES ambao matokeo yake yalitangaza Januari 2017, alishikilia nafasi ya 7.


Lakini tutajaribu kufafanua ni kwa nini watafiti wa CIES walifikia uamuzi huo ambao kwa wengi unaonekana wa kushangaza.


Ronaldo si kinda tena


Tathmini ya thamani ya mchezaji sokoni huzingatia mambo mengi. Moja muhimu ni umri.


Ronaldo anakaribia kugonga miaka 33.


Ronaldo si mzee wa kustaafu lakini anafikia ukingoni wa maisha yake ya uchezaji.


Kwa mujibu wa Chama cha Wachezaji wa Soka ya Kulipwa England kwa mfano, umri wa kawaida wa wachezaji kustaafu huwa miaka 35.


Wachezaji walio na umri wa juu kimsingi huumia zaidi, na wanapoumia, huchukua muda mrefu kupona.


Hili ni jambo ambalo klabu huzingatia zinapomnunua mchezaji.


Neymar anaongoza kwa thamani


"Sijaelewa ni kwa nini watu wengi hivi wameshangaa," anasema Dkt Raffaele Polli, mmoja wa watafiti wanaoongoza katika CIES ameambia BBC.


"Ronaldo ni jina kubwa katika soka na mchezaji mzuri sana, lakini anakaribia kutimiza miaka 33 na miezi ya karibuni kiwango chake cha soka kimeanza kushuka. Wachezaji wachanga mara nyingi thamani yao huwa juu.


"Kusema kweli, thamani yake kwa mchezaji wa umri wake ni ya juu."


Kuna uwezekano mdogo sana kwamba Paris Saint-Germain wangetoat $263m kumnunua Neymar Agosti iwapo mchezaji huyo angekuwa na umri zaidi ya umri wake wa sasa, miaka 25.


Kwa kweli, ni wachezaji wanne pekee wa zaidi ya miaka 29 ambao wamo orodha hiyo ya 100 bora, na Ronaldo ndiye ana umri wa juu zaidi.


Wengine ni Messi, LuĆ­s Suarez (Barcelona) na Gonzalo HiguaĆ­n (Juventus).


Lionel Messi ndiye mchezaji pekee aliyezidisha miaka 29 kwenye 10 bora


Kasi ya mchezaji kufunga mabao


Lionel Messi ana miaka 30 na ndiye wa pili kwa thamani, thamani yake ikiwa $242.8m?


Mbona? Moja ya sababu za mchezaji huyo wa Argentina kuwa na thamani ya juu ni kutoshuka kwa kiwango chake, na mwendelezo wa kasi ya ufungaji mabao.


Messi amefunga mabao kumshinda Ronaldo msimu huu (20 na Ronaldo 16), pamoja na kusaidia ufungaji wa mabao mengi (tisa dhidi ya matatu).


Aidha, kinyume na mwenzake wa Ureno, ligini ufungaji wake haukushuka ukilinganisha na msimu uliotangulia.


Ronaldo aliyetikisa wavu mara 25 La Liga 2016/17 msimu huu amefunga mara nne pekee.


Messi anakaribia kufunga bao lake la 20.


Kujifunga kwenye klabu


Jambo jingine linalozingatiwa ukikadiria thamani ni jinsi mchezaji amejifunga kwa klabu ya sasa.


Hakuna wachezaji wengi ambao wamekaa klabu moja kama Ronaldi.


Alihamia Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009.


Licha ya uvumi mara kwa mara kwamba anaweza kuhamia England au Ufaransa, amesalia Real Madrid.


Hii imeathiri thamani yake sokoni.


Sababu ni rahisi - kupanda sasa kwa bei ya wachezaji. Mwaka 2009, uhamisho wake ulikuwa wa juu zaidi duniani alipohamia Real. Kwa sasa, bei yake ni ya sita katika orodha ya wachezaji walionunuliwa ghali zaidi.


Harry Kane alifunga mabao 56 mwaka jana akichezea klabu na taifa


"Si kwamba Ronaldo amepoteza thamani katika klabu yake, lakini hali kwamba hajahama kwa miaka 10 ina maana kwamba bei yake kwa viwango vya sasa haijulikani," anasema Poli.


Hilo linasaidia kueleza ni kwa nini Gonzalo HiguaĆ­n anamshinda Ronaldo (19 akiwa na thamani ya $135,7 milioni), kwani alinunuliwa na Juventus kutoka Napoli mwaka 2016 kwa zaidi ya $108.1m.


Matokeo ya timu


Ni Mei tu ambapo Real Madrid walishinda La Liga na Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa pamoja, na kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa Ulaya katika robo karne.


Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa sasa, Real walifika hatua ya muondoano kwa urahisi, licha ya kupitwa na Tottenham Hotspur kwenye kundi - na walishinda mechi nyingi Ulaya hatua ya makundi msimu uliopita.


Ronaldo na Real Madrid hawajafana msimu huu La Liga


Real Madrid hata hivyo msimu huu wametatizika La Liga.


Baada ya mechi 18 wamo nafasi ya 4, alama 16 nyuma ya viongozi Barcelona.


"Uchezaji wa klabu pia huchangia thamani ya mchezaji. Msimu huu Real Madrid wamekuwa wanapata kwa wastani chini ya alama mbili kwa mechi La Liga (1.77) ukilinganisha na 2.05 hatua sawa msimu uliopita," anasema mtafiti huyo.


Lakini, hata hivyo, hilo halina maana kwamba klabu zinaweza kutarajia kumnunua Ronaldo kwa bei ya kutupa.


Mreno huyo alilipwa mshahara wa $58m mwaka jana.


Na bado amesalia na miaka mitatu mkataba wake Real Madrid.


Wengine walio na thamani ya juu


Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, fowadi wa Manchester United Romelu Lukaku na kiungo wa kati Paul Pogba, wote wa miaka 24, ndio wachezaji wengine wanaocheza England walio kwenye 10 bora.


Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, aliyetawazwa mchezaji bora zaidi wa kiume duniani na Fifa 2017 yumo nafasi ya 49 kwenye orodha hiyo.


Thamani yake ni euro 80.4m (Ā£71.29m)


Mchezaji mpya wa Barcelona Philippe Coutinho, 25, amewekwa nafasi ya 16 ,thamani yake ikikadiriwa kuwa Ā£33m chini ya bei ambayo Barca walilipa Liverpool kumchukua.


Kipa wa thamani ya juu zaidi ni Marc-Andre ter Stegen, 25, wa Barcelona ambaye thamani yake ni euro 96m (Ā£85.13m) na Samuel Umtiti, 24, ndiye beki ghali zaidi, thamani yake ikiwa euro 101m (Ā£89.56m).


Paulo Dybala, 24, wa Juventus ndiye wa thamani ya juu zaidi Serie A thamani yake ikiwa Ā£155.18m naye Robert Lewandowski, 29, wa Bayern Munich anaongoza kwa wachezaji wa Bundesliga (Ā£94.88m)


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...