Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hatari tano kwa biashara Afrika Mashariki 2018




Kenya inarudi katika hali ya utulivu kisiasa baada ya uchaguzi wa rais uliochukua muda mrefu na uliokumbwa na misukosuko. Hata hivyo changamoto zitaendelea kuwepo mwaka huu kwa mashirika yanayohudumu nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla.


Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kitaalamu Control Risks linalochambua hatari na udhibiti wa hatari za kibiashara na uwekezaji.

Daniel Heal ambaye ni mshirika mkuu wa shirika hilo katika kanda ya Afrika Mashariki, amesema "mwaka 2018 ni mwaka wenye matumaini kwa Kenya na Afrika Mashariki.

Tayari tumeanza kuona imani ya wawekezaji ikirejea taratibu kufuatia udhibiti wa kisasa Kenya na azma katika miradi mipya ya miundo mbinu Kenya na katika kanda hiyo kwa jumla. Tunatarajia hili kuendelea hadi mwisho wa mwaka huu."

Hata hivyo Daniel anasema nchini Kenya, hitaji la kulipa awamu ya kwanza ya mkopo wa fedha za Eurobond ambazo zilikuwa dola milioni 774.8, linapaswa kuishawishi serikali kudhibiti ukopaji na matumizi kabla deni kufikia kiwango cha kutodhibitika.

Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Hatari ya kuchafua sifa

Kenya inayo hamu kubwa ya kukopa, na haijazitambua athari zake kisiasa. Ndivyo anavyosema Daniel. Japo nchi hiyo haijaonesha kuwa itashindwa kuyalipa madeni yake, kuongezeka kwa viwango vya riba na mabenki ya kimataifa kupunguza utayari wao wa kupeana mikopo zaidi, itasababisha upungufu wa matumizi katika sekta ya umma.

Mizozo kuhusu madeni inaibua hatari ya kuharibu jina. Nchi katika eneo hilo zenye uchumi mpana kama Kenya na Ethiopia, zitaepuka mizozo ya madeni. Lakini wawekezaji watakuwa na wasiwasi kuhusu udhibiti wa mikopo kwa muda mrefu. Serikali katika eneo hilo zitahitaji kupiga hatua kubwa katika kudhibiti fedha za umma, zipunguze matumizi na zidhihirishe mikakati ya uwajibishwaji ili kuepuka athari-hasi katika uchumi.

Kuimarishwa kwa miundo mbinu Afrika Mashariki kunatarajiwa kuendelea mwaka 2018. Hata hivyo miradi kati ya mataifa hayo itategemea ushirikiano wa kisiasa ulio imara na wa karibu kati ya serikali za kanda hiyo, hali inayoongeza hatari kisiasa. Kutilia maanani bidhaa za ndani kutaibua hatari kuhusu jina la nchi kwa wawekezaji wa kikanda. Kadhalika masuala ya ardhi na jamii yatahitaji wawekezaji kujitokea kikamilifu kuyasuluhisha ili kuepuka mikwamo yoyote ya utekelezaji  miradi.

Mivutano kati ya serikali kuu ya serikali za kaunti

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Mivutano  kati ya serikali kuu ya Kenya na serikali za kaunti nchini humo huenda ikasababisha hatari za kisiasa. Serikali itahitaji kuimarisha udhibiti na ilenge kuimarisha mazingira mazuri ya kushirikiana na serikali za kaunti ili kuepuka hatari za kisiasa. Pia itahitaji kulenga kuichochea sekta binafsi kwa kuangalia upya viwango vya bima na kuwahimiza wawekezaji binafsi zaidi kushiriki katika miradi ya miundo mbinu. Aidha itahitaji kupunguza vizingiti vya kiserikali.

Hali isiyotabirika ya utungaji sera nchini Tanzania, itaendelea kuzusha changamoto kubwa za kiudhibiti kwa wawekezaji wa ndani na kikanda. Udhibiti wa madaraka wa Rais John Magufuli unaendelea kuwa imara, na uongozi wake wa kiimla na utata wa namna anavyochukulia miswada ya sekta ya uchimbaji madini, kama njia ya kuongeza mapato ya serikali na kukabiliana na upungufu, zinazusha hatari kadhaa za muda mfupi na wastani kwa udhibiti na uwekezaji.

Nchini Uganda mazungumzo kuhusu mrithi wa rais Yoweri Museveni yataendelea. Matukio katika chama tawala National Resistance Movement (NRM) huenda yataibua mkanganyiko katika utungaji sera na kusababisha ucheleweshaji  unaoweza kuathiri biashara.

Nchini Ethiopia, huenda serikali ikakumbwa na maandamano zaidi ikiwa haitapanua uwanja wa siasa na kufanya baadhi mabadiliko katika uongozi. Hali hii itasababisha hatari kwa biashara katika maeneo ya Amhara na Oromia na katikampaka  kati ya Oromia na serikali ya jimbo la Somali.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...