Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TANZANITE

Vigogo Kampuni ya Acacia kortini kwa tuhuma za rushwa

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo.  Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatano Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.  Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania O’mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara.  Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wak...

Licha ya ukuta, 11 wakamatwa wizi wa Tanzanite

Watuhumiwa 11 wamekamatwa na jeshi lapolisi kwa wizi wa madini ya Tanzanite yenye gramu 1110 yenye thamani  ya Tsh 5,551,234.92 yaliyoko ndani ya ukuta wenye kilo meter 24.5 uliojengwa kwenye mgodi wa 'Tanzanite one' ulioko Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Madini ya Tanzanite (Picha ya mtandaoni) Kamanda wa polisi mkoani humo Agustino Senga akizungumza na waandishi wa habari amethibitisha kuibiwa kwa madini hayo na kusema kuwa  watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani Aidha Kamanda Senga amesema kwamba kwa sasa wanafanya tathmini ya kukagua migodi isiyotumika ili iweze kufungwa kutokana na kuwa migodi hiyo ndiyo inayotumika kuwa njia  ya kuingilia kwenye migodi yenye madini. Aidha Kamanda Senga amefafanua kuwa madini hayo yameibiwa na wachimbaji wadogo wadogo na wafanyakazi wa mgodi huo wa 'Tanzanite One' ambao wanauzoefu na mazingira ya maeneo hayo hivyo hutumia uzoefu wao kwa kutengeneza njia za panya maarufu kama mtobozano. Madini hayo yali...