Sure Boy aipa Taifa Stars kuvuna alama tatu katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon 2021 baada ya kuifunga Guinea ya Ikweta mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa ulishuhudiwa Stars wakiutawala kwa asilimia kubwa lakini iliweza kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma bao 1-0. Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa wenyeji kuutawala kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na nahodha wa Stars, Mbwana Samatta aliyekuwa akisaidiana na Simon Msuva kuliandama lango la wapinzani. Samatta alikosa kuiandikia bao Stars dakika ya pili baada ya mpira wake kuokolewa na Mlinda mlango wa Felipe Ovono ambaye alionesha umahiri wake wa kuokoa michomo. Wakati vijana hao wa Kocha, Etienne Ndayiragije wakiendelea kulisakata soka mbele ya watazamaji waliojitokeza kwa wingi kutoa sapoti, walijikuta wakiruhusu bao dakika ya 15 lililofungwa na Petro Obiang ambalo lilidumu hadi mapumziko. Hata hivyo Samatta alikosa nafasi nyingne ya kuisawazishia Stars dakika ya 40 l...