Mamia ya watu wamejeruhiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina Raia 52 wa Palestina wameuawa na wengine 2,400 wamejeruhiwa na wanajeshi wa Israeli katika mapigano mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 2014 katika mpaka wa Gaza, maafisa wa Palestina wanasema. Raia wa Palestina wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa lakini zimechacha leo wakati ubalozi mpya wa Marekani umefunguliwa mjini Jerusalem hatua iliyowaghadhabisha Wapalestina. Wanaitazama hatua hiyo kama Marekani kuunga mkono utawala wa Israel katika mji huo mzima wakati wapalestina wanadai haki ya umiliki wa eneo la mashariki mwa mji huo. Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria. Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye. Israel ilichukua udhibi...