Jerusalem: Mataifa ya kiarabu yalaani hatua ya Marekani


Jana Jumamosi kulishuhudiwa ghasia katika mji wa Nablus, West Bank




Siku ya Jumamosi kulishuhudiwa ghasia katika mji wa Nablus, West Bank

Mataifa ya kiarabu yameitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.





Kwa njia ya taarifa walioitoa kwa kauli moja kwenye mkutano wao Mjini Cairo- Misri, muungano huo umesema kuwa hatua hiyo ni hatari na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na litaitumbukiza mataifa ya mashariki ya kati katika ghasia mbaya.








Israeli: Mahmoud Abbas alifanyia kazi KGB





'Mtego wa kundi la Hamas' wanasa wanajeshi wa Israel





Mawaziri kwenye mkutano huo, sasa wanaiomba jamii ya kimataifa kutaja Mashariki mwa Jerusalem kama makao makuu ya Palestina.





Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Lebanon, Gebran Bassil, amesema kuwa mataifa ya kiarabu, yanafaa kufikiria hatua ya kuiwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi, ili kuizuia kuhamishia makao makuu ya Israeli hadi Jerusalem, kutoka Tel- Aviv.





Bwana Bassil, amesema kuwa, hatua za kidiplomasia na kisiasa, zinafaa kuchukuliwa, kisha kufuatiwa na vikwazo vya kiuchumi na kifedha.





Kumeshuhudiwa tena ghasia katika ukanda wa Gaza na maeneo ambayo yanashikiliwa na Israeli, Magharibi mwa mto Jordan.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU