Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 12.12.2017

MTEULE THE BEST
Olivier Giroud
Olivier Giroud

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, amefichua kuwa anatathmini kuondoka huko Emirates kujiongezea fursa yake ya kuchaguliwa kujiunga na kikosi kinatachoshiriki kombe la dunia. Everton na West Ham wamehusishwa. (Sun)

Lakini Arsene Wenger anasema kwa Giroud hawezi kuuzwa Januari kwa sababu anataka kumpa mshambuliaji huyo muda zaidi wa kucheza uwanjani. (Independent)
Mesut Ozil
Mesut Ozil
Arsenal wanafanya jitihada moja ya mwisho kumshawishi Mesut Ozil kusalia kwenye klabu, wakiwa na matumaini kuwa awamu nyingine mwisho ya mazungumzo kumshawishi mchezaji huo kusalia licha ya Barcelona na Manchester United Kummezea mate. (Daily Mirror)
Real Madrid bado hawajaamua kumpa ofa kipa wa Chelsea raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 25. (Sun)
David de Gea
David de Gea
Real licha ya kuhusishwa na mchezaji wa Manchester United David de Gea, pia wanarajiwa kumsaini kipa wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga, 23 mwezi Januari. (Marca)
Mwandishi ambaye alishikiana na Mourinho kwenye kitabu cha hivi majuzi anaamini kuwa Manchester United itamsainia Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid msimu ujao.(Daily Express)
Diego Lopez
Diego Lopez
Crystal Palace wana uhakika wa kufikia makubaliano ya kumsaini kipa wa Espanyol Diego Lopez, 26. (Daily Mirror)
Meneja wa Leiceser Claude Pue amefichua kuwa alijaribu kumsaini Demarai Gray wakati akiwa huko Southmpton. (Daily Star)
Sam Allardyce atawauliza kikosi cha kwanza cha Everton ikiwa watataka kuwa kwenye klabu hiyo kabla ya kukamilisha mpango wa kusaini wachezaji wapya mwezi Januari. (Guardian

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU