MTEULE THE BEST
Doug Jones amakuwa mwanasiasa wa kwanza wa Democrat katika kipindi cha miaka 25 kushinda kiti cha Seneta katika jimbo la Alabama nchini Marekani baada ya kanpeni kali ya kumpinga mgombea wa Republican Roy Moore kwa kura 51-49.
Huku asilimia 99 ya kura zikiwa zimehesabiwa, Bw Moore alikataa kukubali kushindwa Jumanne usiku
Alipambana na kampeni yenye utata ambapo madai yaliibuka kuhusu dhuluma za kimapenzi na wasichana wadogo.
Bw. Moore ambaye amesema kuwa anaamini mapenzi ya jinsia moja yanastahili kuharamishwa amekana mara nyingi madai dhidi yake
Vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Jones ameshinda baada ya asilimia 99 ya kura kuhesabiwa.
Lakini Moore, 70 aliwaambia wafuasi wake kuwa bado mambo hayajakwisha.
Alisema anaamini mwanya wa ushindi utapungua wakati kura zinaendelea kuhesabiwa.
Licha ya Bw. Moore kukataa kushindwa, Rais Trump alimpongeza Bw Jones kupitia mtandao wa Twitter muda mfupi baada ya vyombo vya habari kumtangaza kuwa mshindi
Maoni