MTEULE THE BEST
Hatimaye klabu za Yanga na Simba zimepata wapinzani wao kwenye michuano ya kimataifa msimu wa 2017/18 kupitia droo iliyofanyika leo nchini Cairo nchini Misri chini ya kamati ya utendaji ya CAF.
Mabingwa wa Tanzania Klabu ya Yanga itaanzia nyumbani raundi ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na St. Louis ya Shelisheli. Kama Yanga itaiotoa St. Louis itakutana na mshindi kati ya Al Merreikh ya Sudan na Township Rollers ya Botswana.
Simba SC pia itakuwa nyumbani kuanza raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya klabu ya Gendarmerie Tnale ya Djibouti. Mshindi kati ya Gendarmerie na Simba atakutana na mshindi kati ya El Masry toka Misri na Green Buffaloes wa Zambia.
JKU SC ya Zanzibar itaanzia nyumbani Uwanja wa Amaan, Unguja dhidi ya Zesco kabla ya kusafiri hadi Ndola kwa mchezo wa marudiano. Zimamoto wao wataanzia nyumbani pia dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia na wakivuka hatua hiyo watakutana na Zamalek ya Misri.
Katika droo ya leo jumla ya mataifa nane klabu zake hazijajumuishwa kwenye michuano ya msimu huu. Nchi hizo ni Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome na Principe, Sierra Leone na Somalia
Maoni