SERIKALI KUNUNUA VICHWA VYA TRENI VILIVYOOKOTWA BANDARINI AMBAVYO HAVIKUWA NA MWENYEWE

MTEULE THE BEST


Miezi michache iliyopita kuna vichwa  vya treni 11 vilionekana bandari ya Dar es salaam  vyenye nembo ya Shirika la reli nchini (TRL) ambavyo taarifa ilisema vichwa hivyo havina mwenyewe.

Waziri wa Uchukuzi Prf. Makame Mbarawa amesema Serikali imeamua kuvinunua vichwa hivyo  kwa bei ya chini kutoka dola  3.8 milioni hadi 2.4 milioni.

Waziri Mbarawa amesema serikali imefikia makubaliano na mmiliki kuvinunua Vichwa hivyo 11 ambapo kila kichwa ni Dola Milioni 2.4 ambapo vyote 11 vitagharimu dolla milioni 26.4

Inadaiwa kuwa vichwa hivyo ni vikuukuu vilivyotolewa katika karakana ya TRL Morogoro kwenda kufanyiwa ukarabati nje ya nchi na kurudishwa nchini na kuonekana kana kwamba ni vipya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU