MTEULE THE BEST
Chama tawala nchini Afrika kusini, ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi pia atakuwa na nafasi ya kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Chama tawala nchini Afrika kusini, ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi pia atakuwa na nafasi ya kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Chama cha ANC kitamtangaza mrithi wa rais wa sasa Zuma kuwa kiongozi wa chama Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano mkali wa kuwania uongozi ambao unatishia kukigawa chama hicho ambacho kilianza kama vuguvugu la ukombozi miaka 105 iliyopita, ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1994.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa , mwenye umri wa miaka 65, ambaye kwa kiasi kikubwa anapendelewa na masoko ya fedha, na Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 68, waziri wa zamani na mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika wametamalaki katika mpambano huo.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa
Sarafu ya Afrika kusini ya rand imekuwa imara kwa asilimia mbili baada ya mahakama kutoa hukumu kwamba maafisa waandamizi katika majimbo mawili walioonekana kumuunga mkono Dlamini-Zuma walichaguliwa kinyume na sheria na hawataruhusiwa kuhudhuria mkutano huo.
"Ishara za mapema za ushindi kwa Cyril Ramaphosa, ambaye anapendelewa na wawekezaji zaidi, ametoa usaidizi kwa sarafu ya rand," John Ashbourne , mtaalamu wa uchumi wa Afrika katika taasisi ya Capital Economics amesema.
"Lakini wakati Ramaphosa anaungwa mkono kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho, matokeo yataamuliwa na watu wa ndani kisiasa, ambao huenda wakaamua kumuunga mkono mpinzani wake mfuasi wa siasa wa mrengo wa kushoto, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Nkosazana Dlamini-Zuma
Ramaphosa alishinda kwa wingi wa kura za kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama, lakini wajumbe katika mkutano huo ulioanza JumamosiDisemba (16-12 hadi 20.12.2017) mjini Johannesburg hawafungwi na kura alizopigiwa na tawi la chama cha ANC lililomteua kuwa mgombea wao, ikiwa na maana kwamba bado haiko wazi iwapo anaweza kushinda nafasi hiyo.
Ramaphosa ameongeza hivi karibuni ukosoaji wa serikali ya Zuma iliyogubikwa na kashfa, wakati Dlamini-Zuma amesema umuhimu wake anauweka katika kuboresha uwezo wa Waafrika waliowengi.
Waungaji mkono Ramaphosa
Kwa waungaji wake mkono, mafanikio ya Ramaphosa kibiashara yanamfanya kuwa katika nafasi nzuri ya jukumu la kubadilisha hali ya uchumi wa nchi hiyo inayokabiliwa na ukosefu wa nafasi za ajira kwa asilimia 28 ya watu pamoja na kupunguziwa viwango vya uwezo wa kukopa.
Mkutano wa ANC akihutubia mwenyekiti Jacob Zuma
Kwa upande mwingine, Dlamini-Zuma anaonekana kuwa mpiganaji imara dhidi ya kutokuwa na uwiano wa Waafrika na wazungu hali ambayo uhasama wake unaoelekezwa katika makampuni makubwa umewatisha wawekezaji nchini Afrika kusini.
"Matokeo ni vigumu kutabiri. Hii inaleta hali mbaya ya sintofahamu ambayo inaakisi kwa kiwango kikubwa hali mbaya ya sarafu ya rand, " Elizabeth Andreae, mchambuzi katika benki ya Commerzbank amesema katika taarifa.
Ukuaji wa uchumi katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa wa viwanda barani Afrika umekuwa wa kusua sua kwa miaka sita iliyopita, na kiwango cha watu wasio na kazi inakaribia viwango vya juu kabisa.
Wachambuzi wanasema kinyang'anyiro cha kuwania uongozi wa ANC umefanya hali kuwa ngumu kuweza kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kuboresha huduma za jamii.
Rais wa zamani wa halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma
Zuma alitoa utani katika chakula cha usiku kwa wajumbe wa ANC katika mkesha wa mkutano huo mkuu na kusema kwamba "imekuwa uzoefu unaostahili" na kwamba anasubiri kwa hamu kuondoka madarakani kama kiongozi. Anatarajiwa kutoa hotuba yake ambayo si rasmi sana mwanzoni mwa mkutano huo mkuu wa chama. Anabakia kuwa kiongozi wa taifa hadi 2019.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 75 amekana madai kadhaa ya rushwa tangu alipoingia madarakani mwaka 2009 na amenusurika mara kadhaa katika kura za kutokuwa na imani nae bungeni.
"Watu wanasubiri kwa hamu kuondoka kwake," mchambuzi wa masuala ya kisiasa Prince Mashele amesema katika taarifa yake aliyoiandika katika gazeti moja
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Lebo
SIASA SOUTH AFRICA
Lebo:
SIASA
SOUTH AFRICA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni