MTEULE THE BEST
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, na kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) imefanya uteuzi wa mwisho kwa wanachama wa CCMwatakagombea katika Uchaguzi wa Ubunge katika Majimbo matatu.
Katibu Mwenezi wa NEC-Itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kwamba katika kikao hicho kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wa chama cha CCM ambaye pia ni Rais , Dkt. John Pombe Magufuli kilipitia majina ya walio omba dhamana na kwa kuzingatia misingi ya maadili, uchapakazi, uwakilishi bora na wenye tija kwa wananchi.
Taarifa hiyo imesema kamati kuu imewateuwa Monko Justine Joseph, Mgombea wa CCM Jimbo la Singida Kaskazini,Ndg. Damas Daniel Ndumbaro, Mgombea wa CCM Jimbo la Songea Mjini na Ndg. Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa, Mgombea wa CCM Jimbo la Longido.
Maoni