MAGUFULI: MJUE MNA MIAKA MITANO YA KUUMIA TENA

MTEULE THE BEST







Mwenyekiti wa (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa endapo watachagua viongozi kama waliokuwepo awali watambue watapata shida kwa miaka mingine mitano.






Magufuli amesema hayo leo Disemba 10, 2017 akiwa Makao Makauu ya nchi mjini Dodoma alipohudhuria Mkutano Mkuu wa tisa wa UVCCM Taifa ambapo amewataka vijana wa chama hicho wasiogope kufanya maamuzi yenye kuleta mabadiliko katika safu ya uongozi wa Umoja huo kwa kuwa viongozi waliokuwepo tayari wameonyesha kuwa na dosari na kuwakosesha nafasi vijana wengi kuweza kupewa nafasi katika serikali ya awamu ya tano.

"Mwenyekiti mtakaye mchagua, Makamu Mwenyekiti na uongozi wote wa vijana mtakaouchagua leo hao ndiyo watakuwa washauri wangu wakubwa ila mkichagua kama wale ambao hawakunishauri hata kwa kuniletea majina ya kuteua kwenye nafasi zenu, mkachagua tena katika mwaka huu mjue mna miaka mitano mingine ya kuumia" alisisitiza Rais Magufuli 

Aidha Rais Magufuli aliwataka vijana hao kutowachagua viongozi wa UVCCM ambao wanatumia fedha kutaka kupata nafasi ndani ya umoja huo wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

*NUKUU ZA NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA   KWENYE MKUTANO MKUU WA 9 WA UMOJA WA  VIJANA WA CCM (UVCCM)*

Disemba 10, 2017.
Dodoma.

1. "Ni ukweli usiopingika kuwa, uhai na ustawi wa taifa lolote duniani ni vijana, hii inatokana na sababu moja vijana ni kundi kubwa" JPM

2. "Chama kinapokuwa na vijana wengi walio hamasika ndio usalama wa chama na taifa " JPM

3. "Napenda mfahamu ujana pekee haikufanyi uwe hazina ila ili uwe hazina inakupasa uwe mzalendo, muadilifu, nidhamu, utu, mchapakazi, mtii, mwenye kupenda kujielimisha na mwenye udhutu wakuleta fikra mpya na siyo kijana legelege".JPM

4. "Kijana ambaye ni mpenda rushwa, mwizi, fisadi, tapeli, mtumia madawa ya kulevya hana mchango wowote kwa taifa na hata kwa chama".JPM

5. "Uchaguzi huu ni muhimu sana kwa sababu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ni chombo muhimu sana katika chama". JPM

6. "Muelekeo wa Umoja wa Vijana tuliokuwa tunaujua, siyo muelekeo tulionao sasa".JPM

7. "Ni lazima wajumbe mlioko hapa mumtangulize Mungu mbele, na mtambue jukumu lenu kwa Vijana wote wa Tanzania".JPM

8. "Nitashangaa sana kama leo mtaniletea Mwenyekiti aliyewahonga, kuwahonga ni kushusha thamani yenu, na ni dalili ya kuonesha hatokuwa kiongozi mzuri".JPM

9. "Mwenyekiti wa Vijana anayetakiwa ni mmoja tu, makabila ya watanzania ni zaidi ya 120 hamuwezi kuchagua kwa kabila na mkifanye hivyo  hamtafanikiwa kupata kiongozi".JPM

10. "Mkachague viongozi waadilifu, wanyenyekevu, wachapakazi, wenye kuchukizwa na rushwa watawavusha. Ninyi muwaelekeze viongozi pakwenda siyo
wao wawaelekeze pakwenda".JPM

11. "Umoja wa Vijana limekuwa ni kundi la kuwazuia vijana wengine wasiingie,  kila mwenye uwezo amekuwa akiwekewa vigingi vya kila aina". JPM

12. "Nawaomba Ndugu zangu vijana msitengeneze ukuta na vijana wenzenu taifa hili ni lenu wote". JPM

13. "Viongozi wakiwa wanyonge na wachini wanakuwa wanyonge zaidi, Vijana wa CCM niwaombe mjiamini mmekuwa wanyonge sana".JPM

14. "Ifike wakati viongozi wastaafu mrudi kwenye jumuia hii hata mfanye nao mikutano ya kuwahamasisha na kuwatia moyo". JPM

15. "Hii bodi ya Umoja wa Vijana iondoke bodi hii haitusaidii".JPM

16. "Viongozi mtakao wachagua na mliochaguliwa fanyeni tathimini ya mali za Umoja wa vijana ziwe kwenye daftari moja, hapo ndipo mtakuwa mnaweza kujitegemea". JPM

17. "UVCCM iwe sauti ya vijana, mtetezi wa vijana, kimbilio, chemchem ya fikra na chuo cha kuandaa vijana katika uongozi kwa chama na serikali "JPM

18."Chagueni wagombea wenye sifa na uwezo". JPM

19."Tuanzishe ukurasa upya wa Umoja wa Vijana nawapenda sana UVCCM nina wahitaji katika kuleta maendeleo ya Nchi yetu". JPM

20. "Na waahidi kila penye nafasi vijana hatutawasahau".JPM
.
21." Vijana muwe wenye kujenga hoja na msibweteke, anzisheni miradi tutawasaidia". JPM

22."Ukijituma watu watakuona tu".JPM

23. "Nataka Umoja wa Vijana wenye muelekeo wakushika dola".JPM

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU