Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TANESCO YA OMBA RADHI KWA WATUMIAJI

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashin amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
Bw. Dashina amefafanua kwamba kufuatia taharuki ya tatizo la kimtandao lililotokea jana kupelekea watu kupata shida katika ununuzi wa umeme Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema tatizo la kimtandao ambalo lilianza jana kufuatia hitilafu katika mfumo limeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo wanatarajia kumaliza tatizo hilo ndani ya siku chache.
ā€œJana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundiā€ amesema Dashina
Aidha Bwana Dashina amesema mpaka sasa wataalamu wanaendelea na zoezi la ukarabati ambalo limekamilika kwa asilimia kubwa ambapo wanaendelea na uhamishaji mitambo kutoka ofisi zao za zamani na kuweka kwenye ofisi mpya.
Kwa upande wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka.
Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka watanzania kuwa na imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia  kama inavyohitajika na kuongeza kwamba tukio hilo la jana limesimamisha shughuli nyingi ambazo zimerudisha nyuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuwahakikishia wananchi tatizo hilo kumalizika haraka iwezekanavyo.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...