Fidel Castro aliitawala Cuba kama taifa lenye mfumo wa chama kimoja kwa takriban nusu karne Tawala za kijamaa zilianguka kote duniani , lakini Castro aliendelea kupeperusha bendera nyekundu karibu na maadui wake wakubwa, Marekani. Kiongozi huyo mwenye utata alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa ambaye aliirejesha Cuba mikononi mwa watu. Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwazima wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima bwanyenye , Angel MarÃa Bautista Castro y Argiz, ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania. Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe. US LIBRARY OF CONGRESSImage captionBatista (Kushoto) aliungwa mkono na Marekani Castro alisoma katika shule ya kikatol...