Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UCHUKUZI

NDEGE YA TANZANIA AIR-BUS A220 YATUA ACCRA, KUTUA KESHO DAR ES SALAAM

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini. Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.   Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.   “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona T...