MTEULE THE BEST Viongozi wa Ulaya wakutana kuzungumzia 'mfumo wa dijitali' Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Tallinn, Estonia, kuzungumzia "mfumo wa dijitali" licha ya kugubikwa na mjadala uliotokana na mapendekezo ya rais wa Ufaransa kuhusu mustakbali wa Umoja huo. Majadiliano yatakayoanza jioni ya leo (Septemba 29) yanatarajiwa kugubikwa na pendekezo la Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa la jinsi ya kutozwa ushuru makampuni makubwa makubwa ya kidijitali mfano wa Apple au Google, yanayotuhumiwa kutolipa ipasavyo kodi ya mapato. Ufaransa inapendelea kuona makampuni makubwa makubwa mfano wa Google au Apple yakitozwa ushuru unaostahiki badala ya mtindo unaotumika hivi sasa wa kutozwa katika nchi moja tu ya Umoja wa Ulaya, mfano wa Ireland au Luxemburg, kodi ya mapato kwa shughuli za kibiashara walizofanya katika nchi zote za Umoja wa Ulaya. Mada hiyo italeta malumbano katika mkutano huo wa kilele, ingawa haijaorodheshwa katika ajenda ya mazungu...