Mwanamume akamatwa akiwa ameficha dhahabu sehemu ya choo cha nyuma

MTEULE THE BEST

Sri Lankan officials presenting the smuggled itemsHaki miliki ya pichaSRI LANKA CUSTOMS
Image captionMwanamume akamatwa akiwa ameficha dhahabu sehemu ya choo cha nyuma
Mamlaka nchini Sri Lanka zimemkamata mwanamume ambaye alijaribu kusafirisha dhahabu na vito vya karibu kilo moja, alivyokwa ameficha sehemu ya choo cha nyuma.
Maafisa wa forodha walipata gramu 904 za dhahabu yenye thamani ya dola 29,370 ndani sehemu ya choo cha nyuma.
Mwanamume huyo raia wa Sri Lanka mwenye umri wa miaka 45, alikuwa safarini kwenda nchini India, lakini akasimamishwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Colombo.
Polythene packagesHaki miliki ya pichaSRI LANKA CUSTOMS
Image captionMwanamume akamatwa akiwa ameficha dhahabu sehemu ya choo cha nyuma
Kumekuwa na visa kama hivyo miaka ya hivi karibuni.
Watu hununua dhahabu maeneo kama Dubai na Singapore ambapo bei ni ya chini na kisha kuisafirisha hadi India ambapo bei yake ni ya juu.
Maafisa wa forodha waliiambia BBC kuwa walimshuku mwanamume huyo kwa sababu alikuwa akiotembea kwa njia isiyo ya kawaida.
Sri Lankan officials presenting the smuggled itemsHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionMwanamume akamatwa akiwa ameficha dhahabu sehemu ya choo cha nyuma
Vifaa vya kutambua chuma kisha vinatambua mkoba uliokuwa umefungwa mfuko wa plastiki na kufichwa sehemu ya choo cha nyuma.
Wiki iliyopita mwanamke mmoja raia wa Sri Lanka alipatwa na maafisa wa forodha akiwa ameficha gramu 314.5 za dhahabu sehemu ya choo cha nyuma.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU