Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BONGO FRAVA

Msanii wa The Mafik akamatwa kwa wizi

Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi. Wasanii wanaounda kundi la The Mafik, Hamadai (kushoto) Mbalamwezi (kati kati) na Rhino (kulia) Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin. Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu. Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea. East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kama...

Chemical:- Natafuta mwanaume" -

Msanii wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical, ametangaza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa mkweli ili awe naye kwenye mahusiano kwa malengo ya kufunga naye ndoa. Chemical amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo atatokea mwanaume ambaye atakuwa 'serious', hatosita kuwa naye. Kabla ya kufikia uamuzi huo Chemical alielezea juu ya kitendo cha kumtosa Stereo, na kusema kwamba msanii huyo alikuwa anamjaribu lakini aligundua hakuwa mkweli kwake, ndio maana ameamua kutafuta mtu ambaye atakuwa 'serious' naye. 'Wanaume wengi wanaumiza, kuna watu wanahisi Chemical haingii kwenye mahusiano, mimi ni mdada jamani naingia kwenye mahusiano, moyo wangu uko very delicate hivyo sipendi kuumizwa moyo, lakini akitokea mwanaume wa ukweli ambaye hatamuumiza Chemical, niko tayari kupenda na kupendwa, Stereo alikuwa anataka kunichezea, sijui alikuwa anataka kujaribu, hakuwa serious, mimi nilijifanya kumkataa kidogo tu akapat...

Mwaka mchungu na mtamu kwa Diamond

Toka mwaka 2009 hadi sasa Diamond Platnumz amekuwa akifanya vizuri kimuziki na kipindi chote hicho ameweza kushinda tuzo za ndani na za kimataifa pia. Kabati lake lina tuzo kubwa zaidi ya 10 kama Channel O Music Video Awards, HiPipo Music Awards, MTV Europe Music Awards/WORLDWIDE ACT AFRICA/INDIA, MTV Africa Music Awards, African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na nyinginezo.  Kwa mwaka huu amefanya mengi makubwa na mazuri ingawa amekuwa na changamoto kubwa kwake.Chini nimeweka yale aliyofanikiwa na yale yalimpatia changamoto kwa huu.  1. Muziki Wake   Ni mwaka ambao Diamond Platnumz amejikuta nyimbo zake tatu zikifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Diamond hakuwa msanii wa kufungiwa lakini mwaka huu upepo huo umempuliza vilivyo.  February 28, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ni zile ambazo hazikupaswa kuchezwa kwenye vyombo vya habari....

Mimi sipendi kutumia kondomu" - Chemical

Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma zake , Chemical ameweka wazi kuwa yeye siyo muumini wa kutumia kinga (kondomu) ndiyo maana mara nyingi anapenda kuwa kwenye mahusiani na mtu ambaye ni muaminifu. Kupitia kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook EATV, Chemical amesema hayo wakati alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho mara yake ya mwisho kutumia kinga. "Mara ya mwisho kutumia kinga wakati nafanya mapenzi ni muda kidogo, ila kiukweli mimi sio shabiki wa kinga kabisa. Mambo ya kinga kinga mimi hapana ndiyo maana napenda sana kuwa na mtu aliyetulia. Chemical" Pamoja na hayo Msanii ameweka wazi kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mtu yoyote kwa kuwa ameamua kuchagua kutengeneza maisha yake na kuhofia kuumizwa moyo wake