Msanii wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical, ametangaza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa mkweli ili awe naye kwenye mahusiano kwa malengo ya kufunga naye ndoa.
Chemical amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo atatokea mwanaume ambaye atakuwa 'serious', hatosita kuwa naye.
Kabla ya kufikia uamuzi huo Chemical alielezea juu ya kitendo cha kumtosa Stereo, na kusema kwamba msanii huyo alikuwa anamjaribu lakini aligundua hakuwa mkweli kwake, ndio maana ameamua kutafuta mtu ambaye atakuwa 'serious' naye.
'Wanaume wengi wanaumiza, kuna watu wanahisi Chemical haingii kwenye mahusiano, mimi ni mdada jamani naingia kwenye mahusiano, moyo wangu uko very delicate hivyo sipendi kuumizwa moyo, lakini akitokea mwanaume wa ukweli ambaye hatamuumiza Chemical, niko tayari kupenda na kupendwa, Stereo alikuwa anataka kunichezea, sijui alikuwa anataka kujaribu, hakuwa serious, mimi nilijifanya kumkataa kidogo tu akapata mwanamke, akamvisha mapete manini, alikuwa anataka tu aniumizeā, amesema Chemical.
Chemicla ameendelea kusema kuwa licha ya kwamba Stereo alionekana kutokuwa serious, alifanikiwa kumpandikiza hisia kwani alikuwa akimfanyia mazuri.
ā'He was so gentle' alivyokuwa akinifuata nini, alinifanya mpaka nianze kuona aibu, unajua mimi sina aibu, lakini yeye baada ya siku mbili kashapata bebe, kashafunga ndoa, mimi kiukweli natafuta mwanaume ambaye yuko 'serious'ā, ameongeza Chemical.
Maoni