Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer
Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania.
Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja.
Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka.
Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam.
Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia moja, makundi ya watetezi wa haki za binadamu na wanasiasa wa vyama vya upinzani.
Azimio hilo limeikumbusha serikali ya Tanzania juu ya majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufuata makubaliano ya kimataifa waliyoyakubali katika kulinda haki na utu wa kila mwananchi wake katika hali yake.
Mabadiliko ya sheria
Umoja wa Ulaya na nchi wanachama watafanya kila wawezalo ili kuhamamisha nchi zinazoendelea wanawakubali wapenzi wa jinsia moja na unyanyapaa au unyanyasaji dhidi ya watu hao unapungua huku makundi ya watetezi wa haki za binadamu wanakuwa salama.
Azimio hilo mpia limezitaka mamlaka za Tanzania kubabili sheria za mtandaoni, mawasiliano ya kielektroniki na posta halikadhalika maudhui ya kwenye mtandao. Huduma za vyombo vya habari kuwa na uhuru wa kujieleza na kufuata viwango vya kimataifa katika kutetea haki za binadamu.
Azimio hilo linataka serikali ya Tanzania kufanya mabadiliko ya sheria, sera na kuondoa vipingamizi vyote vya huduma na taarifa kwa wanawake ,wasichana au akina mama wanaojifungua katika umri mdogo .
Pia wametaka kauli ya rais Magufuli kukataza msichana yeyote atakayejifungua akiwa shuleni hatoruhusiwa kuendelea na masomo, inapaswa kurekebishwa.
Wamemtaka rais wa Tanzania kuiwezesha Tume ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo kufanya kazi yake vile inavyostahili ili kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani nje ya nchi.
Wagunge hao pia wanaitaka "Tanzania kuwaachia huru wanasiasa waliopo gerezani."
Azimio hilo limesisitiza umuhimu majadiliano hayo ili kuifanya Tanzania kujidhatiti katika kuweka mazingira mazuri kwa kila mtu bila ubaguzi wowote.
Inaitaka serikali ya Tanzania "kuacha kutumia mabavu katika kutatua mgogoro uliopo kwa wamasai."
Mamlaka za Tanzania ypia zimetakiwa "kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya na wanaharakati wa kisiasa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na makualiano ya kimataifa."
"Umoja wa Ulaya utaendelea kuwa karibu kuangalia namna ambavyo haki za binadamu zinalindwa nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu kuwa salama."
Maoni