Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KLABU BINGWA AFRICA

SIMBA KUJUA MBIVU AMA MBICHI 28/12/2018 CAIRO

mteulethebest Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi. -Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup. -Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45. -Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12. -Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabw...

Simba yaicharaza Mbabane Swallows FC Kipigo cha mbwakoko

Timu ya Simba imeanza vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwakuapiga Mbabane Swallows FC 4-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.  Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane.  Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1.  Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.  Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza

Klabu bingwa Africa: Kinnah Phiri kuwinda Simba

Mbabane Swallows wamkabidhi Kinnah Phiri  mtihani wa Simba Kocha wa zamani wa Mbeya City, Kinnah Phiri amekabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu ya Mbabane Swallows katika mechi dhidi ya Simba. Phiri amepewa jukumu hilo la muda mfupi kutokana na kocha mkuu wa Mbabane Swallows, Thabo Vilakati kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi nne kutoka CAF kwa kosa la kumpiga muokota mpira. Simba itapambana na Mbabane Swallows katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumatano.