Philippe Coutinho Winga wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho - ambaye kwa sasa yupo Barcelona ya Uhispania- anasema hana mpango wa kurejea kwenye ligi ya Premia. Coutinho, 26, ambaye ni nyota pia wa timu ya taifa ya Brazil alijiunga na Barca Januari 2018. (Mirror) Real Madrid wanatarajiwa kutangaza dau la kumnunua kipa wa Chelsea raia wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 24. (Teamtalk) Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa klabu ya Athletico Paranaense ya nchini Brazil Bruno Guimaraes, 21, iwapo watafamikiwa kuchomoka kwenye marufuku ya kufanya usajili. (Mail) Real Madrid wanamatumaini kuwa wakala Mino Raiola atamshawishi mchezaji wake Paul Pogba, 26, ahamie timu yao kutoka Manchester United. (Marca) AC Milan wanamtaka kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino kumrithi Gennaro Gattuso kushika mikoba ya timu hiyo na watampatia kitita cha pauni milioni ili afanye usajili wa wachezaji mwishoni mwa msimu huu. (Mirror) Kablya ya kutua Spurs, Mauricio Pochettino alikuwa meneja wa Espan...