Makardinali 133 wapiga kura wamewasili Roma na mada nyingi zinajadiliwa
Makardinali wanaoendelea na maadalizi katika Mkutano wao,wapo wanajiandaa vema kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa uchaguzi ujao na wakati huohuo mkutano wa 10 asubuhi Mei 5,mijadala yao ilihusu hali ya Kanisa na matumaini yao ya siku zijazo. Vatican News Jumatatu tarehe 5 Mei 2025, Makardinali wameendelea na mkutano wa kumi katika kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu ujao wa uchaguzi wa Papa mpya na kuendeleza mijadala yao kuhusu hali ya Kanisa na matumaini yao ya siku zijazo. Msemaji mkuu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican, Dk. Matteo Bruni, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba Makardinali 179, wakiwemo makardinali 132 wapiga kura, walishiriki katika Mkutano Mkuu wa kumi. Katika taarifa yake alibainisha kwamba Makardinali wote wapiga kura 133 wapo mjini Roma, kabla ya mkutano utakaoanza Jumatano tarehe 7 Mei 2025. Mkutano wa 10 wa makardinali (@VATICAN MEDIA) Kwa upande wa Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, aliliambi...