Ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Eritrea unatarajiwa kuwasili katika nchi jirani ya Ethiopia kwa mazungumzo kuhusu juhudi za amani na kufufua matumaini ya kumalizika ugonvi uliodumu muda mrefu kabisa barani Afrika. Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema mapema mwezi huu yuko tayari kutekeleza masharti yote ya makubaliano ya amani ya mwaka 1998-2000 yaliyomaliza ugonvi wa nchi hizo mbili, akiashiria uwezekano wa kupatiwa ufumbuzi mvutano kuhusu mpaka wa nchi hizo mbili. Rais Isaias Afwerki wa Eritrea akasema wiki iliyopita, anakaribisha kile alichokiita "risala za maana" kutoka Ethiopia na kuamua kutuma ujumbe wa kwanza rasmi wa serikali yake kuwahi kwenda Addis Abeba baada ya kupita miongo miwili . Ujumbe wa Eritrea unawaleta pamoja mshauri wa rais Yemane Gebreab, waziri wa mambo ya nchi za nje Osman Saleh na mwakilishi wa Eritrea katika Umoja wa Afrika-hayo ni kwa mujibu wa kituo cha matangazo kinachomilikiwa na serikali nchini Ethiopia. Wanajeshi ...