Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali za Africa (AFCON) zinazotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri. Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliyebebwa na wachezaji. Shrikisho la soka nchini TFF limethibitisha taarifa hiyo, ikisema kuwa CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali. Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la kwanza ni USD 29 ambayo ni sawa na takribani sh 66,700 za Kitanzania, tiketi za daraja la pili ni USD 18 ambazo ni sawa na sh 41,403 tiketi za daraja la tatu ni USD 6. Katika hatua ya makundi, Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja la kwanza ni USD 35 ambayo ni takribani sh 80,521 kwa daraja la pili ni USD 24 na daraja la tatu ni ...