Tanzania sasa itahitajika kuwafunga Uganda na kuomba Lesotho wafungwe na Cape Verde ili wao wafuzu
Ndoto za Tanzania kushiriki mashindano ya kandanda kwa timu za taifa bara la Afrika (Afcon) zimekumbana na dhoruba kali.
Timu ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars hapo jana jioni, Novemba 18 ilihitaji alama tatu dhidi ya Lesotho ili kufuzu katika fainali hizo zitakazopigwa mwakani Cameroon kwa mara ya kwanza toka mwaka 1980.
Stars inayonolewa na nyota wa zamani wa Nigeria Emmanuel Amunike iliingia dimbani huku mashabiki wake wakiwa na Imani kubwa juu ya timu yao.
Laiti Stars ingepata ushindi wa namna yeyote ile wangefikisha alama nane ambazo Cape Verde na Lesotho wasingeweza kuzifikia.
Tayari Uganda the Cranes wamefuzu kupitia kundi hilo la L kwa kufikisha alama 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyengine yeyote.
Uganda ilifuzu baada ya kuifunga Cape Verde goli 1 bila majibu. Hayo yalikuwa matokeo ambayo Watanzania walikuwa wakiyaombea sababu Cape Verde ilisalia na alama zake nne.
Kitumbua cha Tanzania kiliingia mchanga katika dakika ya 76 kwa goli la kichwa la Nkau Lerotholi.
Baada ya matokeo hayo, sasa Lesotho imefikisha alama 5 sawa na Tanzania huku Cape Verde akishuka mpaka mkiani kwa alama zao 4.
Ili Tanzania wafuzu itabidi waifunge Uganda katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo utakaopigwa mwezi wa Machijijini Dar es Salaam na kuomba Cape Vede waifunge Lesotho.
Matokeo ya Tanzania kufungwa yameibua hisia tofauti japo si siri kuwa kila Mtanzania ameumizwa moyoni.
Baadhi wametaka watu kutulia na kuelekeza nguvu kwenye mchezo ujao dhidi ya Uganda.
✔@zittokabweKwa Watanzania na wapenzi wa soka, ninajua tumeumizwa sana na matokeo ya leo. Hata hivyo hatupaswi kuvunjika moyo kwani Bado tuna nafasi kubwa kwenda #AFCON2019. Kwa wachezaji wa #Taifastars mimi binafsi Bado nina matumaini nanyi. Mungu anataka tushindie nyumbani. Tutashinda
713
160 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
Wapo ambao wanataka Taifa Stars warudi na kwenda kubangua korosho. Mmoja anayetaka adhabu hiyo itekelezwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
✔@jokateMKubangua korosho kunawahusu aisee.
1,040
227 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @jokateM
Mashabiki na baadhi ya wachambuzi wanambebesha mzigo wa lawama kocha Amunike wakiamini hakupanga kikosi kizuri ambacho kingeweza kuleta ushindi. Mmoja anayeamini hivyo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kigwangalla.
Dr. Kigwangalla, H.
✔@HKigwangalla
Leo nimechukua muda kwa shauku na uzalendo mkuu kufuatilia timu yangu ya Taifa, presha niliyokuwa nayo ni ya hatari, mara tunakoswa koswa, mara paap, tumelizwa; na hapa nipo namsubiria Bwana Emmanuel Amunike kama hivi...
484
165 people are talking about this
Maoni