Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TANZIA

Tanzia: sita wafariki kwa ajali Morogoro

Watu sita wamefariki dunia kwa kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, ambapo miongoni mwa waliofariki ni msanii maarufu wa muziki wa mchiriku na singeli kutoka kundi la 'Jagwa', Jack Simela. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro, baada ya gari lao dogo lililokuwa likitokea kwenye mazishi mkoani humo kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo, amethibitisha kupokea miili sita na majeruhi wawili, na kusema kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri hospitalini hapo. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijawekwa wazi, baada ya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro kugong mwamba. Jack Simela alikuwa ni muimbaji kiongozi wa kundi la Jagwa Music ambalo ni maarufu kwa muziki aina ya mchiriku, muziki ambao umekuwa ukipendwa na mataifa ya nje ikiwemo Ujerumani, ambako ndiko mara nyingi yeye na kundi lake walikuwa wakienda kufanya matamasha.         ...

Injinia Alphonse Augustino Cherehani: Asimulia vipi alivyopatikana hai siku 3 baada ya kuzama MV Nyerere?

Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima. 'Siku kama siku nyingine' Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora. Kawaida wakazi wa kisiwa cha Ukara hufurika gulioni kujipatia mahitaji mbalimbali na siku hiyo ilikuwa vivyo hivyo. Kabla ya safari kama kawaida alikagua chombo (MV Nyerere) zikiwemo Injini zake ...

Rais wa Tanzania afiwa na dada yake

Rais Magufuli alipoenda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Dada yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Hapo jana Rais Magufuli alienda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika hospital hiyo ya Bugando na rais alisema kwamba hali ya dada yake sio nzuri. Bi.Monica Magufuli alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25

Watu 20 wafariki dunia katika ajali ya barabarani Mbeya, Tanzania

Takriban watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha zaidi ya magari matatu mkoani Mbeya, kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Ajali hiyo ilitokea katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya. Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40. Mnamo 14 Juni, watu 13 wakiwemo vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya. Aprili, watu wanane waliokuwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah walifariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi katika eneo la Igodima. Gari hilo lililokuwa likitokea Chunya kwenda Mbeya mjini, lilikuwa na abiria tisa waliokuwa wakienda katika msiba wa ndugu yao. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoan...

Watu 10 wafa kwa kugongwa na gari kimakusudi nchini Canada

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema shambulio hilo ni baya na la kijinga, ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Kanada. Waziri Mkuu Trudeau ameonyesha huruma zake kwa wale wanaohusika na mkasa uliotokea. Amesema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii. Bwana Trudeau amesema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu, na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake. Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau Waziri wa usalama wa umma nchini Canada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili  tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa usalama wa umma nchini Kanada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili tah...

Mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush aaga dunia

Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92. Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92. Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush. Bi Bush ambaye alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi. Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani. Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani. Barbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa miula miwili kama rais wa 43 wa Marekani. Katika tanzia alisema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakin...

Watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

MTEULE THE BEST Watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam. Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam. Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule. “Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa. Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhus...

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki

Ramani ya Kenya Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki. Mwanasiasa huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 85. Ken, kama alivyojulikana nchini Kenya ameaga dunia katika Hospitali moja ya kibinafsi ya Karen, iliyoko Jijini Nairobi. Ken Matiba ambaye ni maarufu katika siasa za ukombozi wa pili wa kisiasa nchini Kenya, baada ya ile ya Uhuru miaka ya 1950s na 1960s. Mwanasiasa huyo maarufu ambaye alitatiza pakubwa siasa za Rais wa awamu ya pili nchini humo mzee Daniel Toroitich Arap Moi, alizaliwa Juni Mosi mwaka 1932 - na akafariki Jumapili April 15 ya mwaka huu wa 2018. Alizaliwa katika Wilaya Muranga, iliyoko maeneo ya katikati mwa Kenya. Alikuwa mwanasiasa ambaye daima alikuwa akitabasamu, na mkereketwa wa kutetea haki za kibinadamu na kuwepo kwa demokrasia nchini humo. Aliwania kiti cha urais mwaka wa 1992, lakini akaibuka wa pili, nyuma ya Daniel Toroitich Arap Moi. Kenneth Stanley Njindo Matiba, ambaye ...

Dada yake mwimbaji maarufu Mowzey Radio aliyefariki wiki iliyopita amekamatwa kama mtuhumiwa katika kesi ya kaka yake

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe Polisi nchini Uganda wamemkamata mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu Mowzey Radio, aliyefariki kutokana majeraha aliyoyapata baada ya mzozo uliotokea kwenye kilabu moja ya usiku '' De Bar'', iliyopo katika mji wa Entebbe. Wakati wa mazishi yake, mama yake Jane Kasumba aliwalaani wauaji wake imeripotiwa katika magazeti ya Daily Monitor. Amenukuliwa akisema: Nimeumizwa sana, sana. Lakini kinachoniumiza zaidi ni kwamba sikuwaona waliomuua mwanangu. Ninawalaani waliomuua mwana wangu. " "Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzey Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo chake. Radio, ambaye jina lake halisi Moses Ssekibogo, alifariki kutokana na majeraha yaliyoto...

Mwanamke achomwa hadi kufa kwa 'kukataa' uchumba India

MTEULE THE BEST Maafisa wa polisi katika mji wa kusini mwa India wa Hyderabad wanasema kuwa wamemkamata mwanamume mmoja baada ya mwanamke mmoja kuchomwa hadi kufa wakati wa mgogoro Picha ya mtu aliyavalishwa pete ya uchumba Maafisa wa polisi katika mji wa kusini mwa India wa Hyderabad wanasema kuwa wamemkamata mwanamume mmoja baada ya mwanamke mmoja kuchomwa hadi kufa wakati wa mgogoro. Sandhya Rani, mwenye umri wa miaka 25 alikuwa anaelekea nyumbani wakati aliposhambuliwa siku ya Alhamisi , polisi iliambia BBC. Watu walikimbia kumsaidia bi Rani lakini alifariki akielekea hospitalini. Mshukiwa huyo , Karthika Vanga , 28, ni mfanyikazi mwenzake wa zamani. Alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na bi Rani hadi miezi michache iliopita, polisi liliambia ripota wa BBC Deepthi Bathini. Wakati alipomkaribia siku ya Alhamisi wawili hao walionekana wakijibizana kabla ya mwanamume huyo kuchukua mafiua ya taa, na kumwagia mwilini na kumchoma moto , polisi walidai. Walisema ...

Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo

MTEULE THE BEST Image caption Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul. Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua. Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu. Image caption Picha yake iliwekwa hospital mjini Seoul Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul. Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.

JWTZ wazungumzia vifo vya Wanajeshi 14

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania limesema kikundi chake cha ulinzi na usalama kilichopo DRC kwaajili ya kutekeleza jukumu la ulinzi na amani kilivamiwa na Waasi waliojilikana kuwa ni ADF na kusababisha mauaji kwa wanajeshi 14. Amesema kwamba tukio hilo lilitokea katika eneo la kambi iliyopo daraja kwenye mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamango mpakani mwa nchi ya Uganda Kaskazini Mashariki ya wilaya ya Beni Jimbo la Kivu Kaskazini. Akithibitisha mauaji hayo muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema shambulio hilo lakuvamiwa lilizusha mapigano baina ya kikundi hicho na kile cha waasi na yalidumu kwa takribani masaa kumi na tatu (13) na kusababisha vifo vya askari wa Tanzania 14 na wengine 44 kujeruhiwa na askari wawili bado hawajulikani walipo ambapo jitihada zaidi za kuwatafuta zinaendelea. Amesema shambulizi la tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Desemba lilikua baya zaidi k...

TANZIA: Walinda amani wa Tanzania wauawa DR Congo

MTEULE THE BEST Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba walinda amani 14 wa muungano huo waliuawa na wengine 53 kujeruhiwa baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kati ya waliouawa, angalau wanajeshi 12 walitoka Tanzania. Katibu mkuu huyo ameshutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita. Ameitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa. Wanajeshi zaidi wametumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi. Bw Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni. "Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC. "Taarifa za mwanzo mwanzo eneo la shambulio eneo la Kivu...

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika wa bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai ameongoza  mamia ya wakazi wa Songea mkoani Ruvuma kwenye mazishi ya aliyekuwa  mbunge wa jimbo la Songea  mjini marehemu Leonidas Gama aliyefariki Novemba 23 nyumbani kwake Likuyufusi  mjini Songea.

Picha Kutoka Eneo la Ajali ya Ndege iliyoua watu 11 Ngorongoro Arusha

Jeshi la Polisi Arusha limepata miili ya watu 11 waliofariki kwenye ajali ya ndege ndogo ya Coastal Aviation iliyotokea November 15, 2017 katika eneo la Embakazi Wilayani Ngorongoro. Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na kuchukua abiria watano jumla ikawa na abiria 10 na Rubani akiwa ni mtu wa 11 kwenye ndege hiyo na kuelekea Ngorongoro.

Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita

Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine 41 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza. Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi. Mkoa wa Kagera ni eneo linalowahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani kama Burundi. Baadhi ya wakimbizi hao walikuwa wanajeshi ambao waliacha silaha zao katika baadhi ya makambi. Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi amesema tayari timu ya upelelezi imetumwa katika eneo hilo kuchunguza sehemu ambapo bomu lililipukia. Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu. "Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, weng...