Ramani ya Kenya
Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.
Mwanasiasa huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Ken, kama alivyojulikana nchini Kenya ameaga dunia katika Hospitali moja ya kibinafsi ya Karen, iliyoko Jijini Nairobi.
Ken Matiba ambaye ni maarufu katika siasa za ukombozi wa pili wa kisiasa nchini Kenya, baada ya ile ya Uhuru miaka ya 1950s na 1960s.
Mwanasiasa huyo maarufu ambaye alitatiza pakubwa siasa za Rais wa awamu ya pili nchini humo mzee Daniel Toroitich Arap Moi, alizaliwa Juni Mosi mwaka 1932 - na akafariki Jumapili April 15 ya mwaka huu wa 2018.
Alizaliwa katika Wilaya Muranga, iliyoko maeneo ya katikati mwa Kenya.
Alikuwa mwanasiasa ambaye daima alikuwa akitabasamu, na mkereketwa wa kutetea haki za kibinadamu na kuwepo kwa demokrasia nchini humo.
Aliwania kiti cha urais mwaka wa 1992, lakini akaibuka wa pili, nyuma ya Daniel Toroitich Arap Moi.
Kenneth Stanley Njindo Matiba, ambaye alifanya kazi na na utawala wa Kenya, amewahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri kuu ya shirika la ndege nchini humo, mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini humo- KFF, muasisi na mwenyekiti wa Kenya Football League, gavana wa shule ya upili Kirongo, naibu mwenyekiti wa shule ya upili ya Alliance High, mwenyekiti wa chama tawala wakati huo wa KANU wa tawi la Mbiri, naibu mwenyekiti wa Kanu tawi la Wilaya ya Murang'a, na mwenyekiti shupavu wa kitaifa wa chama cha Kanu.
Matiba, ambaye ni mwanabiashara maarufu, alikuwa mwanakamati mkuu wa kitaifa wa shirika la wamiliki wa hoteli nchini humo na mmiliki wa gazeti maarufu la upinzani wa la The People.
Ken Matiba aambaye alifariki saa 12 na dakika 10 Jumapili 15 mwaka 2018, ndiye muanzilishi wa vuguvugu la mikutano ya Saba Saba, ya mwaka 1990 na 1997.
Kenneth Stanley Njindo Matiba, aligonga vichwa vya habari vya mikutano ya Saba Saba, hasa ule wa kwanza kabisa uliofanyika Julai 7, mwaka 1990, lakini alikamatwa na akafungiwa gerezani, bila ya kufikishwa mahakamani.
Yeye na Rais wa awamu ya tatu nchini humo, Mwai Kibaki, walikuwa katika msari wa mbele wakati wa siasa za upinzani za mwaka 1997.
Wawili hao walikuwa miongoni mwa matajiri wakumbwa nchini humo, lakini Matiba alipotesa sehemu kubwa ya rasilimali yake.
Mawakili wake, wakiongozwa na wakili Paul Mwite, wamefaulu kuwasilisha kesi mahakamni, ambapo serikali ya Kenya inafaa imlipe Jumla ya shilingi, milioni 945 za Kenya, sawa na Dola milioni 9 za kimarekani
Maoni