Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MBOWE AMTELEKEZA LISSU UBELGIJI








Wabunge Saed Kubenea, Anthony Komu wawa chanzo cha mateso ya mwenzao





-Awasusia wamhudumie kwa kusema wameingilia kati mgonjwa wake





-Atangaza kumsusa na kuiagiza kamati kuu yake isijihusishe naye kwa lolote





-Amehifadhiwa Ubelgiji kwa Mtanzania anayeishi huko, nyumba moja ya vyumba viwili na sebule anaishi Lissu, mke wake na watu wengine saba





– Anaishi maisha magumu ya mateso na fedheha kubwa  asiyowahi kuyafikiria huku akienda hospitali na kurudi





-Wabunge, wanachama wagawanyika wakimshangaa Mbowe kuzuia mabilioni ya chama kumsaidia kiongozi wao muhimu





– Chama kinapokea Bilioni 4.5 za ruzuku kila mwaka, milioni 680 ya michango ya wabunge kila mwaka lakini kimemtelekeza mbunge wake





Na Shaaban Ismail





HALI ya huduma za kimatibabu na maisha kwa jumla ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, nchini Ubelgiji, zimezidi kuwa ngumu na sasa mbunge huyo anaishi kwa msaada wa wasamaria wema walioko nchini humo.





Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kabla hajapatwa na mkasa wa kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area ‘D’, mkoani Dodoma, Septemba 9, mwaka jana, alikuwa tayari anatajwa kuwa amejipanga kugombea uenyekiti CHADEMA huku akiungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge wenzake ndani ya chama hicho.





Jambo hilo linadaiwa kutomfurahisha Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambaye anaendelea kukitumikia chama hicho kwa nafasi hiyo kwa mwaka wa 14 mfululizo sasa.





Taarifa za uhakika ambazo zinatoka ndani ya chanzo muhimu katika CHADEMA zinasema kuwa mpaka sasa chama hicho kimejitoa kumsaidia mbunge huyo na kwamba anaishi kule kwa hisani tu ya Mtanzania mmoja (jina tunalihifadhi kwa sasa).











Tundu Lissu akiwa na mke wake sebuleni kwa mtanzanianchini ubelgiji





Kwa mujibu wa taarifa hizo, tangu  Lissu awasili ubelgiji, hajapokea hata senti moja kutoka katika chama chake zaidi ya michango iliyokuwa ikichangishwa kutoka kwa wanachama wa chama hicho, marafiki pamoja na Chama cha Wanasheria Tanzaganyika (TLS) ambacho hadi kufikia juzi, mbunge huyo alikuwa ndiye rais wake.





Chanzo chetu cha uhakika kilichomo ndani ya kamati kuu ya CHADEMA kinasema kuwa Mbowe alikiagiza chama chake kutompa Lissu msaada wa aina yoyote.





Pia anadaiwa kuwaonya wabunge watakaojitia kimbelembele kumsaidia Lissu kwamba wajiandae maana siku zao za ubunge zinahesabika huku yeye mwenyewe akijitoa rasmi  kushiriki kutoa aina yoyote ya msaada.





Taarifa zinasema kuwa wabunge; Saed Kubenea (Ubungo-CHADEMA) na Anthony Komu (Moshi Vijijini-CHADEMA) ndiyo pekee waliosusiwa kumhudumia mwanasheria mkuu wao huyo wa chama kwa kile kinachodaiwa kujitia kwao kiherehere kwa kumsafirisha Lissu kwenda Ubelgiji bila ruhusa na ridhaa ya Mbowe.





“Komu na Kubenea ndio waliofanya mpango wa kumpeleka Lissu Ubelgiji. Sasa Mwenyekiti Mbowe amekasirika sana, anasema kwanini wameingilia kati na kujifanya wanajua zaidi yake, ndio akazuia chama kisimsaidie msaada wowote”. kinaeleza chanzo chetu





Saidi Kubenea, Mbunge wa Ubungo – CHADEMA





Pamoja na michango ya wanachama na makusanyo ya kadi za wanachama wapya wanaojiunga kila siku na chama, CHADEMA pia hupokea wastani wa Sh. milioni 369 kila mwezi kutoka serikali kuu kama ruzuku ya uendeshaji wa chama hicho.





Jambo linaloshangaza ni kwanini Lissu atelekezwe Ubelgiji huku akiishi kwa mateso makubwa wakati chama chake kinakusanya mabililioni ya shilingi kila mwaka.





“CHADEMA tunapokea ruzuku ya karibu bilioni 4.5 kwa mwaka kutoka serikalini. Na miongoni mwa fedha hizo, zimo zinazotokana na jasho na ushawishi wa Tundu Lissu kwa wapigakura. Nashangaa sana Mbowe kukifanya chama kama mali yake na sasa hivi Lissu amesusiwa mtu binafsi Ubelgiji, waulize Komu na Kubenea watakwambia kama huniamini”. anasema msiri huyo





Msiri wetu ameongeza kuwa kila mbunge wa CHADEMA wa kuchaguliwa huchanga kwa lazima kuanzia Sh. 500,000 mpaka milioni 1 kwenye chama.





Aidha, mbunge wa viti maalumu anachanga kwa lazima kati ya Sh. milioni 1.5 na milioni 2 kila mwezi kulingana na matukio ya kisiasa ya mwezi husika sambamba na mchango wa lazima uliowekwa na kanuni za chama ambapo kwa michangoo ya wabunge wa viti maalum pekee chama hicho kinakusanya wastani wa Sh. milioni 86 kila mwezi huku michango ya wabunge wa kuchaguliwa, inakusanya wastani wa milioni 18 mpaka 22 kila mwezi





Msiri aliongeza kusema kuwa: “Hakuna aliyeamini! Mwenyekiti anaiambia kamati kuu kuwa yeye ameshatoa mchango wake vya kutosha. Sasa anawaachia wanaojidai kujua zaidi waendelee na Lissu na hakuna hata senti moja chama itatoa mpaka wapate adabu”.





Lissu alipelekwa Ubelgiji kwa awamu ya tatu ya matibabu yake, ambayo kwa hivi sasa mbunge huyo ameingia katika hatua ya kufanya mazoezi ya viungo zaidi ili arudishe siha ya mwili wake baada ya matibabu ya awamu ya kwanza na ya pili yaliyofanyika Nairobi, nchini Kenya





Tangu Lissu apelekwe Ubelgiji, ni Kubenea tu, ndiye ambaye anayeelezwa kuwa anahusika kumsafirisha kwenda nchini humo akishirikiana na Komu ambaye ndiye aliyepata kwenda kumjulia hali.Anthony Komu, Mbunge Moshi Vijijini – CHADEMA





Mbowe inaelezwa kuwa hajawahi kwenda hata siku moja na taarifa zinasema pia kuwa wala hana mpango wa kwenda huko kutokana na kinachoitwa “kisasi cha kisiasa”.





Mara kadhaa kumekuwa na maneno ya chini chini miongoni mwa wabunge na wanachama wa CHADEMA wakimsema Lissu kuwa ndio mtu sahihi kwa sasa kuukwaa uenyekiti wa chama hicho kutokana na ukweli kwamba mwenyekiti wao amefanya kazi kubwa kukifikisha chama hapo kilipo na sasa anapaswa kuruhusu damu mpya ikiongoze jambo linalosemwa kutokumfurahisha mwenyekiti wa chama hicho.





Mpango huo unaoratibiwa kumuweka kando Mbowe na kumkabidhi Lissu chama, unaelezwa kuungwa mkono na wabunge wengi zaidi ndani ya chama hicho tofauti na wachache wanaotaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wao.





Kwa kawaida wabunge wengi wa kuchaguliwa, mara baada ya kumalizika kwa kampeni za uchaguzi na kuapishwa, hujikuta wakilipa madeni yanayotokana na uchaguzi.





Hali hiyo imekuwa ikiwa wajikute wakikopa kiasi kikubwa cha fedha katika mabenki mbalimbali kwa dhamana ya Bunge ili kulipa madeni na kufanya masuala mengine ya kimaendeleo.





Vitendo hivyo vimekuwa vikiwafanya wabunge wengi kupokea kiasi kidogo cha fedha kama mshahara baada ya kukatwa na benki.





Jambo linamfanya Lissu kuwa miongoni mwa wabunge hao  na hivyo kujikuta akiteseka kutokana na kukosa fedha za kujikimu.





Jamvi la habari linawaahidi wasomaji wake kuendelea kuwahabarisha kuhusiana na jambo hili katika matoleo yajayo




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...