Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi.
Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi.
Bwana Mugabe alizishutumu kampuni za kigeni za kuchimba madini kwa ''kuiba'' na ''kusafirisha'' katika mahojiano na runinga ya taifa 2016.
''Kampuni hizo zimetuibia utajiri wetu'' , alisema. Akiongzea kuwa wizara ya fedha ilipokea $15bn pekee.
Haijulikani iwapo raia huyo mwenye umri wa miaka 94 atakubali kufika mbele ya kamati hiyo ya bunge.
Alilazimishwa kujiuzulu mwezi Disemba iliopita kufuatia mapinduzi ya kijeshi na bado anahudumiwa na serikali kama rais wa zamani
Maoni