Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kuna mipaka kati ya uhuru wa kujieleza na Maadili?

MTEULE THE BEST
Watumiaji wa mitandao wamekuwa wakilaumiwa kukiuka maadiliHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionWatumiaji wa mitandao wamekuwa wakilaumiwa kukiuka maadili
Mitandao ya kijamii ni majukwaa ya kutoa maoni. Jamii imekuwa ikitumia majukwaa hayo kujieleza kwa kutumia sanaa, kutoa hotuba, kutoa mawazo au maoni, kwa njia ya maandishi, picha au michoro.
Mitandao kama Facebook, Tweeter, Instagram, Snapchat, Jamii forum, Whatsapp na mingine mingi imetumika kwa muda mrefu kutimiza azma hiyo.
Hata hivyo watumiaji wamekuwa wakikosolewa kwa kiasi kikubwa kuhusu namna wanavyoitumia mitandao hiyo.
Ukuwaji wa matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa watanzania hasa vijana umeifanya serikali ya Tanzania kuweka Sheria ya Kukabiliana na uhalifu Mitandaoni mwaka 2015 ambayo tangu wakati huo imekuwa ikikosolewa kwa kuwaandama watumiaji wa kawaida wa mitandao hiyo.
Ukiukaji wa maadili
Wiki moja baada ya kampeni ya #ifikiewazazi kusambaa mitandaoni nchini Kenya, mamlaka ilianza kuwatafuta vijana waliokuwa wamepiga picha mbaya kwenye maeneo ya umma.
Vijana kadhaa walijikuta matatani baada ya kukamatwa wakipiga picha mbaya hadharani na baadhi yao wanashikiliwa katika kituo cha polisi Nairobi.
Ripoti zinaonyesha kuwa vijana walikua katika bustani ya Michuki jijini Nairobi wakipiga picha chafu, wakifanya vitendo vinavyoelezwa kuwa vya 'kihuni'.
Polisi wamekuta picha chafu na dawa za uzazi wa mpango kwa vijana hao wadogo.
''Walikuwa wakifanya vitendo ambavyo mtazamaji hawezi kuvivumilia. Tumewakamata wasichana wadogo na kijana mdogo wa kiume wote chini ya umri wa miaka 18, alisema mkuu wa polisi wa kituo hicho, Robinson Thuku.
Hashtag hiyo #ifikiewazazi - ilileta ghadhabu mitandaoni juma lililopita, na ililenga vijana hao ambao walikuwa wakipiga picha mbaya ili picha hizo ziwafikie wazazi.
Sheria ya Tanzania kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao
Mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video iliyosambaa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kitandani akicheza na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto pia na mwanamke mwingine ambaye hajajulikana,picha zinazoelezwa kuwa hazina maadili.
Waziri wa habari, sanaa na michezo Tanzania, Dkt Harrison Mwakyembe amewaambia wabunge ni matokeo ya sheria mpya za mitandao zilizopitishwa mapema mwezi uliopita.
Serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani.
''Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao wamekuwa wakifanya uhuni uhuni ndani ya mitandao jana tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Diamond tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha na vile vile Nandi naye imebidi apelekwe Polisi kuhojiwa tunaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.
"Nitoe wito kwa vijana mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu, hii nchi ina utamaduni wake tunahitaji kuulinda'' amesema Mwakyembe.
Nandi pia ni mwanamuziki nyota, ambaye picha yake ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa na mwanamuziki wa kiume Billnas ambaye inadaiwa kuwa mpenzi wake akiwa kwenye nguo yake ya ndani sambamba na mwenza wake kitandani.
Sheria hizi mpya za mitandaoni zimetungwa kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya mitandao hiyo, huku wakosoaji wakisema kuwa sheria hizi zipo kwa ajili ya kukandamiza uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.
  • Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa kupitia katika mfumo wa kompyuta ponografia au ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu.
  • Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika.
  • Iwapo ni uchapishaji kuhusiana na ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja; au
  • Ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni thelathini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka kumi au vyote kwa pamoja.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...