Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Bashar al-Assad arudisha tuzo aliyopewa na Ufaransa


Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus.

Syria imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya LĆ©gion d'honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kwa taifa ambalo limekuwa 'mtumwa' wa Marekani.


Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia.


Ufaransa hivi majuzi ilijiunga na Ufaransa na Uingreza katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za kinyuklia dhidi ya raia wake.


Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus.



Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu 2001 baada ya kuchukua mamlaka kufautia kifo cha babake.


''Wizara ya maswala ya kigeni imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya LĆ©gion d'honneuri iliopewa rais Assad'', wizara ya kigeni nchini Syria ilisema katika taarifa.


''Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani linalounga mkono ugaidi'', iliongoza.



Bashar al-Assad alipokea tuzo hiyo 2001 kutoka kwa rais wa Ufaransa Jacques Chirac

Takriban watu 3,000 kila mwaka hutuzwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu kwa huduma waliotoa kwa Ufaransa ama kwa kutetea haki za kibinaadamu, uhuru wa kujieleza ama sababu kama hizo.


Marekani , Uingereza na Ufaransa zilishambulia vifaa kadhaa vya serikali ya Syria siku ya Jumamosi ili kujibu matumizi ya silaha za kemikali katika mji wa Douma, ambao ndio mji wa mwisho uliokuwa ukikaliwa na waasi katika jimbo la mashariki mwa Ghouta nje ya Damascus.


Zaidi ya watu 40 walifariki katika shambulio hilo la Aprili 7 kulingana na wanaharakati wa upinzani, wafanyikazi wa uokoaji na maafisa wa matibabu.


Serikali ya Syria imekana kutumia silaha za kemikali na kusema kuwa shambulio hilo lilipangwa.


Viongozi wengine waliopokezwa tuzo hiyo ni pamoja na aliyekuwa rais wa Tunisia Zine El Abiine Ben Ali 1989 na rais wa Urusi Vladimir Putin 2006.


Kufikia sasa ni rais mmoja pekee aliyepokonywa taji hilo-rais wa Panama Manuel Norriega. Hivi majuzi Nyota wa Hollywood Harvey Weinstein pia alipokonywa tuzo hiyo baada ya kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...